Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

KIUNGO wa zamani wa FC Barcelona, Mhispania Xavi Hernández Creus rasmi amerejea kwenye Klabu hiyo kama Kocha Mkuu, baada ya kufutwa kazi Kocha Ronald Koeman kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu hiyo yenye sifa ya kucheza Soka la Pasi duniani.

Katika mahojiano na Waandishi wa Habari wakati wa utambulisho wake, Xavi amesema “Nafurahi kuwa hapa. Naishukuru Klabu na kila mtu. Ambao wamenipa sapoti mimi kuwepo hapa. Sisi (Barca) ni timu kubwa duniani lazima tufanye kazi kwa jitihada ili kufika mafanikio. Hatuwezi kupata mafanikio kwa kupata sare na kufungwa. Sisi ni Barcelona lazima tushinde kila mchezo”.

Kupitia Mkutano huo na Wanahabari, Xavi amesema anaguswa na timu hiyo ikiwa katika wakati mgumu, ameeleza kuwa licha ya kuwa katika wakati mgumu wanahitajika kufanya vizuri ili kurejea katika hali yao ya zamani ya ubora na kung’ara katika Ligi ya Hispania na mashindano mbalimbali duniani.

“Tunaamini njia pekee ya kushinda na kufanya vizuri ni kucheza soka zuri. Tunajitaji furaha, kushambulia, kucheza mchezo wa wazi, kutawala mchezo na kucheza kwa nafasi, natamani mafanikio makubwa kama ya Kocha Pep Guardiola na Johan Cruyff”, ameeleza Xavi.

Kwa upande wa Rais wa timu hiyo, Joan Laporta amesema wana furaha kwa ujio wa Xavi Hernández kwenye Kikosi chao, amesema hiyo ni historia nyingine kutokana na Kocha huyo aliwahi kucheza katika Klabu hiyo kwa mafanikio makubwa na kufanikisha timu hiyo kutwaa mataji mbalimbali makubwa duniani.

Xavi mwenye michezo 767 alipokuwa FC Barcelona, ametambulishwa Camp Nou mbele ya Mashabiki takriban 9,422 wa Klabu hiyo akisindikizwa pia na Familia yake. Katika historia yake ya Soka akiwa Klabuni hapo ametwaa mataji ya Ligi Kuu nchini Hispania (La Liga) mara 26, Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA CL) mataji 5, Kombe la Dunia la Klabu mataji 3 na Copa Del Rey mataji 31.

Xavi Hernández aliondoka Barcelona mwaka 2015 ambapo alisajiliwa na Klabu ya Al Sadd ya Qatar na kucheza kati ya mwaka 2015-2019 baadae kuwa Kocha Mkuu wa miamba hiyo ya Soka nchini Qatar kati ya mwaka 2019-2021.
Kocha mpya wa FC Barcelona, Xavi Hernández (kulia) akiwa na Rais wa Klabu hiyo, Joan Laporta (kushoto) wakati wa utambulisho wake katika dimba la timu hiyo, Camp Nou, tukio hilo lilishuhudiwa na mashabiki takriban 9,422.
Rais wa Klabu ya FC Barcelona, Joan Laporta akimtambulisha Kocha wa timu hiyo, Xavi Hernández huku familia yake ikishuhudia utambulisho huo uliofanyika Camp Nou. Xavi amerejea Barca kama Kocha Mkuu baada ya kufutwa kazi Kocha Ronald Koeman kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu hiyo.
Kocha wa FC Barcelona, Xavi Hernández akisalimia Mashabiki wa timu hiyo waliojitokeza katika utambulisho wake kwenye dimba la Camp Nou.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...