Na Denis Sinkonde, Songwe
Wajumbe wa halmashauri kuu ya chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Ileje mkoani Songwe wameunga mkono halmashauri kuu ya chama hicho Taifa kufanya mchakato wa uteuzi wa mgombea nafasi ya Uspika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Tulia Ackison.
Mwenyekiti wa chama hicho Hebron Kibona amesema hayo January 21 mwaka huu wakati wa mkutano wa halmashauri kuu ya chama hicho uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Itumba.
Kibona amesema mchakato wa kumpata mgombea mmoja kati ya wagombea 71 walioomba nafasi ya kuteuliwa na chama kuwania nafasi ya Uspika kuongoza muhimili huo wa serikali umekidhi vigezo hivyo kama wajumbe wa halmashauri kuu wilaya wanaunga mkono juhudi za kamati kuu ya CCM Taifa ikiongozwa na mwenyekiti wa CCM Taifa Mh. Samia Suluhu Hassan.
"Kila mwanaccm aliyechukua fomu kuomba kuteuliwa na chama kuwania nafasi ya Uspika wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alikuwa na sifa lakini chama kikaona kwa wakati huu anayepaswa kushika wazifa huo ni Dkt .Tulia ambaye ni naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na mbunge jimbo la Mbeya Mjini ambaye anapaswa kuungwa mkono alisema Kibona".
Katibu wa chama hicho Hassan Lyamba amesema mchakato wa vikao vya sekeritalieti , na halmashauri ya kamati kuu Taifa kwa uamuzi walichofanya kwa kuteua jina la Dkt.Tulia Ackison Mwasasu kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Uspika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao unaungwa mkono na wanaccm wa Ileje hivyo .
"Hakuna mtu ambaye hafahamu uwezo wa Dkt .Tulia Ackison kutokana na uzoefu wake kiongozi tangu ateuliwe kuwa mbunge kuanzia mwaka 2015-2020 na hatimaye kugombea ubunge jimbo la Mbeya mjini na kushinda mwaka 2020 hivyo wabunge wa CCM wampigie kura za ndio alisema Lyamba''.
Mbunge wa jimbo la Ileje mkoani hapa Mhandisi Godfrey Kasekenya Msongwe amesema Kama mbunge wa jimbo la Songwe ameipongeza kamati kuu kumteua Dkt. Tulia Ackison Mwasasu kuwania nafasi za Uspika wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwani uzoefu wake katika nafasi ya Unaibu spika utakuwa chachu ya kulitumikia bunge kwa lengo la kuwaletea watanzania maendeleo.
Mwenyekiti wa jumuiya ya vijana UVCCM Ileje Maon Jeckison Mbuba amesema mchakato uliotumika kumpata mgombea umekidhi vigezo kwa kuepusha rushwa kama ilivyozoeleka kipindi Cha kumpata mgombea kupitia chaguzi mbalimbali.
Kwa kauli moja wajumbe wa kikao hicho wamekubaliana na maamuzi ya kamati kuu chini ya mwenyekiti wake Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia vikao vyote na kufanikisha kukonga mioyo ya watanzania na wanaccm wa Ileje kumpata mgombea pekee Dkt. Tulia Ackison.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...