Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar KWA niaba ya Chama, Ndg. Abdallah Juma Saadalla ametoa maelekezo kwa Makatibu wa CCM wa Mikoa pamoja na Umoja wa Vijana (UVCCM) Zanzibar kuhakikisha wanapanga utaratibu wa wanachama wa CCM na Vijana wa Umoja wa Vijana kujitolea katika ujenzi wa Hospitali za wilaya zinazojengwa katika wilaya zote 11 za Uguja na Pemba.

Naibu Katibu Mkuu ametoa maelekezo hayo leo jumatano 26 Januari, 2022 katika ziara ya wajumbe wa Sekretarieti ya HKT inayoendelea Visiwani Zanzibar, alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Kaskazini A inayogharimu shilingi Bilioni 4.4 iliyoanza kujengwa mwezi Januari mwaka huu na ikitarajiwa kukamilika mwezi Juni, mwaka huu.

Naibu Katibu Mkuu akitoa maelekezo hayo baada ya kukagua na kuridhishwa na ujenzi unaoendelea, ambapo amesema kuwa utamaduni wa WanaCCM ni kusaidia katika maendeleo na ujenzi wa nchi yetu, hivyo akitoa maelekezo hayo amesema,

"Naagiza Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar, tuwalete hapa vijana watekeleze Ilani ya Uchaguzi na kujenga Taifa, na kwa upande wa chama naagiza Makatibu wa Mikoa yote ya Unguja na Pemba kupanga ratiba ya matawi ya CCM katika maeneo husika yawe yanashiriki katika ujenzi wa Hospitali katika wilaya zote za Zanzibar, na hiyo ndio asili tuliokuwa nayo Chama Cha Afro Shiraz Party na TANU na sasa ni CCM"

Nitapita kukagua namna makatibu wa mikoa mlivyoyapanga matawi katika kutekeleza hilo na vijana wa umoja wa vijana wa CCM mnavyotekeleza maagizo haya, Naibu Katibu Mkuu amesisitiza.

Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Unguja Ndg. Ayoub Mohammed Mahmoud akitoa maelezo ya ujenzi wa hospitali Katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, amesema kuwa,

"Katika Mkoa Hospitali ya Kivunge inajengwa ambayo ujenzi unaendelea na unagharimu shilingi bilioni 4.8, na hapa Kaskazini A hospitali inajengwa kwa shilingi bilioni 4.4 na ni eneo ambalo linauhutaji mkubwa wa hospitali ya wilaya."

Miradi hii itachukua miezi sita kukamilika ambapo imeanza mwezi Januari mpaka Juni 2022, Mkuu wa Mkoa ameongeza.

Katika hatua nyingine Naibu Katibu ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kilimo cha umwagiliaji mpunga Kibokwa, mradi wa upanuzi wa gati bandari ya mkokotoni, mradi wa eneo maaluma la viwanda Pangatupu, mradi wa maboresho ya bandari ya bumbwini/Pangapwani, pamoja na kuzungumza na wanachama katika mikutano ya mashina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...