Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo pamoja na mambo mengine ameitaka Serikali kuanza ujenzi wa viwanda vya nguo katika Mkoa wa Simiyu na maeneo mengine ambapo zao la pamba linalimwa kwa wingi.

Katibu Mkuu ameyasema hayo Jumatatu Januari 31 mwaka huu katika ziara maalum ya Sekretarieti ya HKT katika mkoa wa Simiyu yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuhimiza uhai wa chama ngazi ya mashina.

"Ni lazima mtengeneze mazingira yakuwa na pamba inayoanzia hapa na kuvaliwa hapa. Kiwanda kijengwe hapa Bariadi na pamba ichakatwe hapa ili matokea yaonekane hapa, lazima tuweke msukumo viwanda vijengwe hapa, na nguo zinazotokana na pamba yetu kwa sababu ni bora na nguo zitakuwa bora."

Katibu Mkuu ameyasema hayo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Ndg. David Kafulila akieleza mafanikio makubwa wanayotarajia kuyapata katika uzalishaji wa zao hilo la Pamba mwaka huu.

Aidha katika hatua nyingine, Katibu Mkuu ametembelea na kukagua mashamba ya wakulima wa pamba katika wilaya ya Bariadi, maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi za CCM za Matawi na Kata, ujenzi wa Barabara ya Somanda - Isakalyamhela pamoja na Kuhudhuria mkutano wa shina namba 8 kata ya Nkololo.

Katika ziara hiyo Wilayani Bariadi, Katibu Mkuu ameambatana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiongozwa na  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Ndg. Shamsa Mohammed Seifu pamoja na Mkuu wa Mkoa huo Ndg. David Kafulila.


 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Igegu, Bariadi mkoani Simiyu ikiwa sehemu ya ziara ya Ukuaguzi, Usimamiaji, Uhamasishaji na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 – 2025 pamoja na kukagua uhai wa CCM katika ngazi za mashina.

Katibu Mkuu ameongozana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Ndugu David Kafulila (kulia) wakati wa mkutano wa kushiriki kujenga ofisi za CCM, Bariadi mkoani Simiyu ikiwa sehemu ya ziara ya Ukuaguzi, Usimamiaji, Uhamasishaji na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 – 2025 pamoja na kukagua uhai wa CCM katika ngazi za mashina.

Katibu Mkuu ameongozana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akiwa amemshikia kipaza sauti na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Ndugu David Kafulila (kulia) wakati wa kujibu hoja mbali mbali za wakazi wa shina namba 8 Kitongoji cha Idahilo Mjini, Bariadi mkoani Simiyu ikiwa sehemu ya ziara ya Ukuaguzi, Usimamiaji, Uhamasishaji na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 – 2025 pamoja na kukagua uhai wa CCM katika ngazi za mashina.

Katibu Mkuu ameongozana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.



Sehemu ya Wakazi wa Shina namba 8 Kitongoji cha Idahilo Mjini, Bariadi mkoani Simiyu walihudhuria mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo, ikiwa sehemu ya ziara ya Ukuaguzi, Usimamiaji, Uhamasishaji na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 – 2025 pamoja na kukagua uhai wa CCM katika ngazi za mashina.

Katibu Mkuu ameongozana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.



Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu Bi. Shemsa Mohamed akihutubia wakati wa shina namba 8 Idaho Mjini wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo wilayani Bariadi mkoa wa Simiyu ikiwa sehemu ya ziara ya Ukuaguzi, Usimamiaji, Uhamasishaji na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 – 2025 pamoja na kukagua uhai wa CCM katika ngazi za mashina.

Katibu Mkuu ameongozana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.(Picha na CCM Makao Makuu)
 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...