Katika mkuu wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari Dkt Jimmy Yonazi akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau wa kidigitali cha kujadili tathimini ya mahitaji ya taaluma ya TEHAMA
Mratibu wa mradi wa Tanzania ya kidigitali Honest Njau kutoka wizara ya habari mawasiliano na teknolojia ya habari akielezea mradi huo
Katibu mkuu wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Dkt Jimmy Yonazi akiwa katika picha ya pamoja na maafisa rasilimali watu na wataalamu wa TEHAMA kutoka wizara  mbalimbali
Baadhi ya maafisa rasilimali watu na wataalamu wa TEHAMA wakifuatilia jambo katika kikao cha wadau wa kidigitali cha kujadili tathimini ya mahitaji ya taaluma ya TEHAMA Vero Ignatus,Arusha

Katibu mkuu wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Dkt Jimmy Yonazi   amewataka maafisa rasilimali watu pamoja na wataalamu wa TEHAMA  kuhakikisha wanatambua vipaji na kuviendeleza kupitia uchumi wa kidigitali na mabadiliko ya teknolojia yanayoendelea Duniani.

Dkt. Yonazi aliyasema hayo wakati akifungua kikao Cha wadau wa digitali Cha kujadili tathimini ya mahitaji ya taaluma ya TEHAMA yatayotekelezwa kupitia mradi wa Tanzania ya kidigitali ambapo alisema kuwa  ni wajibu wao kuhakikisha vipaji hivyo vinawapeleka pale wanapopataka kwa TEHAMA kuchangia kukuza uchumi.

“Dunia imebadikika sana na teknolojia ya sasa inabadilika kila siku na cha kwanza ni uelewa wa watu na namna wanavyotumia teknolojia, watu wanazidi kupata fursa ya kutumia TEHAMA katika mambo mbalimbali kwahiyo nyie wataalamu ni lazima muwe wabunifu na kuhakikisha kuwa eneo hili la kidigitali linafikisha nchi tunapopataka,” Alisema Dkt Yonazi.

Alieleza kuwa ni lazima kuwa wanafunzi wa kudumu kwa kuwa tayari kujifunza kila mabadiliko yanapotokea kwasababu mabadiliko yanayoendelea kutokea ni makubwa na yanatokea kila siku na TEHAMA ya nchi haitaendelea kama wao hawatafanya jambo jipya.

“Kila siku muwe wabunifu na wawajibikaji kwa kufanya tafiti  na naamini mafunzo haya yatayotolewa kwa watumishi 500 kutoka tasisi mbalimbali yatakuwa ni chachu kwaajili ya kuleta ubunifu na tafiti zenye tija kwa maendeleo ya watu wa nchi yetu,” Alieleza.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Tanzania ya kidigitali Honest Njau alisema kuwa mradi huo wenye thamani ya Dola milioni 150 ni wa miaka mitano  na upo chini ya ufadhili wa benki ya Dunia ambapo lengo ni kuendeleza na kupata mawasiliano ambayo ni rahisi na na yenye ubora.

Alifafanua kuwa mradi huo wa Tanzania ya kidigitali unalenga kuboresha na kukuza maunganisho ya kidigitali ya ndani, kikanda na Kimataifa ili kufikisha huduma za mawasiliano pamoja na utoaji wa huduma mbalimbali za kidigitali kwa wananchi na kuweza kuboresha na kukuza ubunifu kwenye TEHAMA.

Alisema kuwa mradi umegawanyika kwenye maeneo matatu ambayo mojawapo ni ikolojia ya kidigitali ambapo lengo lake ni kujenga taifa la kidigitali kwa kustawisha mazingira wezeshi katika nyanja za uwekezaji kwenye TEHAMA, na nyingine ni uunganishaji wa kidigitali unalenga kuboresha miundombinu ya mawasiliano ya serikali na kuendeleza jitihada za kupunguza ukosefu wa mawasiliano hususani sehemu za pembezoni mwa nchi na sehemu zisizo na mawasiliano kama vile vijijini.

“Upande wa ikolojia ya kidigitali malengo yake yatatekelezwa kupitia mazingira wezeshi ya kidigitali pamoja na upande wa miundombinu ya kusaidia maendeleo ya TEHAMA na kuimarisha biashara ya kieletroniki lakini pia eneo la uunganishaji wa kidigitali itafanyika katika maunganisho ya serikali na kuendeleza mawasiliano vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara kwa watoa huduma za mawasiliano,” Alisema.

Alifafanua kuwa eneo la tatu ni jukwaa la huduma za kidigitali ambapo eneo hilo litaongeza litaongeza uwezo wa miundombinu ya msingi inayohitajila katika utoaji wa huduma za umma za kidigitali ili kuongeza ufanisi wa shughuli za ndani za serikali na kuendeleza majukwaa ya uzalishaji wa huduma za umma za kidigitali.

“Katika eneo hili la jukwaa la huduma za kidigitali eneo hili litatekelezwa kupitia huduma za kidigitali na mifumo ya uzalishaji, miundombinu ya kuhifadhia Data pamoja na uwelewa  na kujenga uwezo katika masuala ya kidigitali,” Alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...