Na Khadija Seif, Michuziblog

TAASISI ya Kusaidia watu wenye uhitaji Happy Hands Tanzania  wahaidi kuendeleza juhudi za Kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutangaza utalii wa ndani.

Happy hands Wamedhamiria Kwa dhati kuunga Mkono juhudi hizo Kwa Kumleta Mwanamuziki kutoka nchini Sweden  Mahir zein hapa Tanzania na kumpelekea katika Moja ya hifadhi za Wanyama katika Mkoa wa Arusha pamoja na Visiwa vya Zanzibar.

Hata hivyo Mahir zein atakuwepo nchini  Kwa lengo la kutoa burudani mapema mwezi Marchi 12 na kutembelea vivutio vilivyopo nchini kabla ya tarehe rasmi ya Tamasha hilo anatarajiwa kutembelea Mbuga za wanyama zilizopo Arusha.

Hata hivyo taasisi hiyo Kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imempa nafasi Mwanamuziki huyo kutembelea vivutio vilivyopo Visiwa vya Zanzibar.

Mahir zein anatarajiwa kutumbuiza katika Ukumbi wa Dom uliopo Masaki jijini Dar es salaam na viingilio ni shilingi elfu 50.

Aidha, Happy Hands imeomba wadhamini kujitokeza Kwa wingi katika kufanikisha Tamasha hilo na Kwa mwaka huu mikakati Yao ni kuendelea kusaidia wanawake,walemavu pamoja na watoto Kwa kiasi kitakachopatikana katika Tamasha hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...