Makamo  Mwenyekiti wa Familia ya Hayati Mwalimu Nyerere ,Dkt.Joachim Nyerere akizungumza kuhusiana na Tamasha la "JUKANYE" lenye lengo la kusherehekea Miaka ya Muasisi huyo wa Taifa la Tanzania

Na.Khadija Seif, Michuzi TV

FAMILIA ya Muasisi wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wanatarajia kuandaa Tamasha  "Jukanye Festival" kutimiza miaka 100 ya kuzaliwa kwake.

Tamasha hilo litafanyika Aprili 20 mwaka huu Butiama Mkoa w Mara , Musoma kwa lengo la kumuenzi na kushiriki burudani mbalimbali.

Makamo Mwenyekiti wa familia hiyo Dk. Joachim Nyerere amesema Tamasha Hilo litakuwa la siku tatu ambapo kilele kitafanyika Aprili 20 mwaka huu 

"Mwalimu Julius Nyerere alizaliwa Aprili 13 siku hiyo itakuwa ibada  kwa ajili ya kumuomba Mungu, hivyo tumesogeza mbele hadi Aprili 20," amesema.

Dk. Joachim alieleza kuwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikuwa mpenzi wa muziki siku hiyo kutakuwa na Matukio mbalimbali ya burudani.

"Mwalimu Nyerere alikuwa mdau kubwa wa burudani siku hiyo kutakuwa na Matukio tofauti ya burudani ambayo yatapamba tamasha hilo ".


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...