MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na kupinga utaratibu wa kujiuzulu kwa aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai na kusema kuwa, Ndugai alifuata taratibu zote za kujiuzulu ikiwemo kuandika barua kwa mkono ya kujiuzulu kwenda kwa katibu wa Bunge.

Uamuzi huo umetolewa leo Januari 28, 2022 na Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji John Mgeta ambapo amesema.

Katika uamuzi huo, mahakama imesema mbali na barua huyo ya kwenda kwa Katibu wa bunge Ndugai aliwasilisha barua ya pili kwa chama chake kupitia Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Jaji Mgeta amesema ya kwamba hakuna Mtanzania aliyeiona barua ya Spika kujiuzulu bali iliyokuwa ikisambaa ni taarifa kwa umma iliyotolewa na chama chake na si barua ya kujiuzulu.

Baada ya kueleza hayo, Jaji Mgeta akampatia Mbatia nakala kivuli(Copy) ya barua ya Ndugai alivyojiuzulu.

Hata hivyo, Mawakili wa Mbatia wamesema kuwa watakata rufaa kupinga uamuzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...