Kikosi cha KMC FC jana kimeanza maandalizi ya kujiandaa na mchezo wa michuano ya kombe la Azam Sports Federation (ASFC) utakaochezwa siku ya Jumamosi ya Januari 29 mwaka huu dhid ya Ruvu Shootingi ya Mlandizi Mabatini Mkoani Pwani.
Kikosi hicho cha Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu Thiery Hitimana kimeanza kujifua jana ikiwa ni baada ya kurejea kutoka Mkoani Rukwa na Mbeya ambapo ilikuwa kwenye mchezo wa Ligi kuu ya NBC Soka Tanzania Bara dhidi ya Timu ya Tanzania Prisons pamoja na Mbeya kwanza na kufanikiwa kuvuna alama nne na magoli matatu kwenye michezo hiyo.
Katika michuano hiyo KMC FC inajiandaa kufanya vizuri ilikufanikisha adhma ya kuendelea kushiriki kwa mafanikio katika kombe hilo ambapo wachezaji pamoja na benchi la ufundi wameweka mikakati ya kuhakikisha kuwa katika hatua hiyo ya 32 bora inafanya vizuri.
“ Tunafahamu ukubwa na ushindani wa michuano hii, lakini kama Timu tumejipanga vizuri kwani mkakati wetu ni kuhakikisha kwamba tunafanya vizuri na kuendelea kushiriki kwenye michuani hii kwa mafanikio, lakini pia tunafahamu kila Timu ambayo inashiriki inahitaji kufanya vizuri hivyo nasisi tumejipanga pia.
“Tulikuwa kwenye michezo ya ligi kuu ya NBC, ambapo mechi zote tulikuwa ugenini, pamoja na ugumu wa michezo hiyo wachezaji wetu walijituma na kuhakikisha kuwa kama Timu tunarudi na matokeo mazuri na hivyo kufanikiwa kupata alama nne muhimu na magoli matatu hivyo kwa sasa Timu inaelekeza nguvu kwenye michuano ya ASFC.
Imetolewa leo Januari 24
Afisa Habari na Mawasiliano wa KMC FC.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...