Na Damian Kunambi

Kufuatia kilio cha miaka mingi cha wakazi wa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe juu ya uanzishwaji wa miradi ya Liganga na Mchuchuma hatimaye wilaya hiyo imeanza kuingia kwenye historia ya kuanza kwa mradi wa makaa ya mawe katika maeneo ya pembezoni.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya wawekezaji wa ndani wa kampuni ya makaa ya mawe MAXCOAL kujitokeza na kuanza uwekezaji katika kata ya Ibumi kijiji cha Masimavalafu ambacho pia kinapakana na kijiji cha Liugai cha kata ya Luilo.

Mpaka sasa kampuni hiyo tayari imeshapeleka sampuli kwa makampuni mbalimbali ambapo mapokeo yake ni mazuri na wanatarajia  kuanza usambazaji hivi karibuni ambapo kwa kila mwezi wanatarajia kuuza tani zisizopungua laki moja.
Vicent Malima ni Mhandisi wa kampuni hiyo ya makaa ya mawe amesema kwa mujibu wa wataalamu wamedai kuwa makaa yanayochimbwa wilayani Ludewa ni makaa yenye ubora wa hali ya juu kuliko makaa ya maeneo yote hapa nchini hivyo wao tayari wanamiliki eneo la ekari 25 ambazo watachimba kwa miaka isiyopungua 70.

 Aidha kwa upande wa mkurugenzi wa kampuni hiyo Deogratius Charles Amesema mradi huo ni mkubwa sana hivyo wananchi wa Ludewa na maeneo mengine wanapaswa kuchangamkia fursa mbalimbali za kibiashara pamoja na shughuli ndogo ndogo za mgodini.

"Napenda niwahamasishe wakazi wa Ludewa na watanzania kwa ujumla kuja kutumia fursa zilizopo hapa, mwamko umekuwa mdogo sana kuliko matarajio yangu kwani nili
tegemea kwa muingiliano huu wa watu fursa zilizopo zitachangamkiwa vyema", amesema Charles.

Sanjari na hilo mkurugenzi huyo amewatoa hofu madereva wanaokuja mgodini  kubeba mizigo kuwa miundombinu ya barabara ni rafiki kwani mpaka sasa wamesha pakia magari zaidi ya manne ya tani 30 na yamefika salama.

Pamoja na shughuli hizo za uchimbaji makaa kampuni hiyo tayari imeisaidia jamii inayowazunguka kuboresha miundombinu ya barabara ambapo wamechonga barabara ya kupita magari na kujenga daraja katika mto Ketewaka ambalo mpaka kukamilika kwake litatumia zaidi ya milioni 300 unaotenganisha kata ya Ibumi na Luilo.

Ikumbukwe kuwa wananchi wa wilaya ya Ludewa na mkoa wa Njombe kwa ujumla wanaendelea kusubiri kwa hamu kuanza kwa miradi mikubwa zaidi ya liganga na mchuchuma ambapo hivi karibuni msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa alisema miradi hiyo ipo mbioni kuanza kwani tayari wapo katika hatua ya mwisho ya mazungumzo na muwekezaji.
 
Viongozi wa CCM wilaya na kata wakiwasili katika eneo la mradi wa makaa ya mawe unaomilikiwa na kampuni ya MAXCOAL huku wakiongozwa na mhandisi wa kampuni hiyo Vicent Malima
Viongozi wa CCM pamoja na viongozi wa kampuni ya MAXCOAL Ludewa wakiwa wameongozana kukagua eneo la bandari kavu lililopo katika kata ya Luilo.
Eneo la mradi wa makaa ya mawe unaomilikiwa na kampuni ya MAXCOAL
Daraja linalojengwa na kampuni ya makaa ya mawe MAXCOAL linalounganisha kata ya Ibumi na Luilo ambalo ujenzi wake bado inaendelea.
 
 
 
Mhandisi wa kampuni ya Maxcoal Vicent Malima (aliyevaa kofia) akiwaonyesha viongozi wa CCM aina ya makaa ya mawe yanayopatikana mgodi kwao. Kushoto kwake ni katibu wa CCM wilaya Amos Kusakula na katibu wa CCM kata ya Luilo, kulia ni katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Ludewa
 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...