Na Amiri Kilagalila,Njombe

MAHAKAMA ya hakimu mkazi Mkoa wa Njombe imedhamiria kufanya maboresho ya mapinduzi ya kiteknolojia kuelekea mahakama mtandao na kuondokana na utaratibu wa kutumia majalada ya makaratasi kama ilivyozoeleka.

Hayo yamebainishwa na hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya mkoa wa Njombe Liad Chamshama wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria nchini.

Kwa upande wake mtendaji wa mahakama mkoa wa Njombe,Yusu Msawanga amesema katika wiki ya sheria mkoani Njombe,huduma mbalimbali za utoaji wa elimu pamoja na usikilizaji wa kero kutoka kwa wananchi,ambapo wananchi watashiriki zoezi la kujitolea damu salama kwenye viwanja vya stendi ya zamani mkoani Njombe.

Wakati wiki ya sheria ikizinduliwa kwa lengo la kusikiliza kero za kisheria zinazowakabili wananchi, kwa upande wake mwakilishi wa chama cha mawakili wa kujitegemea (Tanganyika Law Society), Wakili Tunsume Angumbwike hapa anasema namna watakavyosaidia kutoa elimu kuhusu masuala ya kisheria ili wananchi watambue haki zao.

Wakati huohuo, Prisca Julius ambaye ni Mratibu wa Damu Salama mkoa wa Njombe ametumia wasaa wa uzinduzi wa wiki ya sheria kutoa wito kwa jamii kujenga utamaduni wa kuchangia akiba ya damu ili kuokoa maisha ya wahitaji wa damu inapohitajika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...