Na.Khadija Seif,Michuzi TV

NYOTA wa Muziki wa Singeli, Khalid Mtumbuka maarufu kama ‘Meja Kunta’ ametambulisha rasmi EP yake ya kwanza aliyoipa jina la ‘Meja Power’ kupitia Kampuni ya Kusikiliza na kupakua  Muziki Mtandaoni ulioenea barani Afrika ya Boomplay.

Akizungumza kuhusu EP hiyo, Meja kunta amesema EP ya “Meja Power" imeandaliwa  na Mtayarishaji  Eyoo Kenny kupitia kupitia studio za Unique sound  na imebeba nyimbo nne ambazo ni "Power, Kama ipo ipo, Mapenzi na Niambie”.

Meja ameongeza kuwa ilikuwa ndoto yake kuachia EP hiyo ambayo hajamshirikisha msanii yeyote ili kuonesha uwezo mkubwa alio nao kama ‘solo artist’.

“Mchakato wa kuachia EP hii ulianza tangu mwaka jana na sasa nafurahi kuona ndoto yangu inatimia,”

Ili kuipa nguvu EP hiyo, Meja Kunta amejipanga kufanya tour katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar ambapo atakutana na mashabiki na kugawa zawadi mbalimbali.

Vilevile kutakua na Mashindano ya kuimba na kucheza nyimbo za Meja Kunta kupitia mitandao ya kijamii ambapo washindi watapewa zawadi mbalimbali.

Meja Kunta ni mojawapo ya wasanii wa Singeli wanaotamba sana nchini Tanzania na muziki wake ulipata mwitikio mkubwa zaidi baada ya kushirikiana na Lavalava kwenye ngoma ya ‘Wanga’ ngoma ambayo ilipata umaarufu kimataifa ambapo Msanii Alicia Keys na Swizz Beatz wa Marekani waliweza kuipa promo nyimbo hiyo.

Mbali na ngoma ya wanga, Mkali huyo wa singeli anatamba na vibao vingine vingi ambavyo vinaendelea kufanya vizuri kwenye soko la Tanzania mpaka sasa ikiwemo Mamu, Madanga ya mke wangu, Simba, Chura Superstar, Kidimbwi na vingine vingi.

Msanii wa Muziki wa Singeli  Khalid Mtumbuka maarufu kama "Meja Kunta" akizungumza na Waandishi Wahabari akitambulisha rasmi EP itakayokua ikipatikana Kwenye Mtandao wa kusikiliza na kupakua Muziki Boomplay ambapo EP hiyo inakwenda Kwa jina la "Meja Power" yenye nyimbo takribani 4

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...