MKUTANO Mkuu Maalum wa Chama cha ACT- Wazalendo, umewachagua Mhe. Juma Duni Haji kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama hicho Taifa, na Mhe. Othman Masoud Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu Mwenyekiti mpya wa Chama hicho kwa upande wa Zanzibar.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi uliofanyika jana huko ukumbi wa Mkikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya ACT Joran Bashange amesema kwamba Mhe. Othman amepata 143 sawa na asilimia 95.83.

Aidha Mwenyekiti mpya wa ACT babu Duni amechaguliwa kwa kura 339 sawa na asilimia 73.06, huku mpinzani wake ndugu Hamad Masoud Hamad akipata kura 125 sawa na asilimia 26.94 ya kura zote halali 468 zilizopigwa.

Pia Mkutano huo ulimchagua ndugu Msafiri Mtemelwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu baada ya kupata kura 216 sawa na asilimia 47 ya kura zote 457 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu huo.

Mhe. Duni anachukua nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti kurithi viatu vya marehemu Maalim Seif aliyefariki Dunia Januari 17 mwaka jana na Mhe. Othman anachukua nafasi ya Babu Juma Duni Haji aliyejuuzulu nafasi hiyo miezi michache iliyopita kwa nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti.

Akitoa salamu za shukrani Mwenyekiti huyo mpya ndu. Juma Dunia haji aliwataka wanachama kumaliza makundi ya uchaguzi na kuhimiza kuwa wamoja katika jitihada za kujenga chama chao.

Aidha alisema kwamba atajitahidi kuanzisha program mbali mbali za kuimarisha chama hicho ikiwa ni pamoja na kufanya ziara za mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar sambamba na kusaidia utolewaji wa mafunzo kwa ngazi mbali mbali za Uongozi wa Chama hicho.

Naye Makamu Mwenyekiti mpya wa Chama hicho kwa Upande wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman aliwataka wanachama kuwa ni mshikamano na ushirikiano na kwamba atajitihadi kuitumikia nafasi hiyo ili kukijenga chama.

Amesema anawashukuru wanachama kwa kumuamini na dhamana hiyo na kwamba atakitumikia chama hicho kwa uwezo wake wote na kuwaasa viongozi wote kuendelea kutumikia vyema chama chao.

Naye Kiongozi Mkuu wa Chama hicho Zito Zuberi Kabwa akitoa salam za shukrani baaada ya kukamilika kwa uchaguzi huo aliwataka wanachama wote kuvunja makundi ya uchaguzi kwavile shughuli hiyo imekishwa rasmi baada ya kupatikana viongozi wapya.

Alikemea kuendelea kuwa na makundi baada ya uchaguzi na kuonya kwamba ni jambo baya ambalo linaweza likaribu chama mustaabali wa chama hicho.

Mkutano Mkuu huo maalum Pia uluhudhuriwa na viongozi wa Vyama Rafiki Kutoka Malawi Zanzibar na vyama vya mbali mbali vya hapa Tanzania ukiwemo uwakilishi wa cha cha CUF. 



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...