CHAMA cha ACT Wazalendo kesho Januari 29, 2022 kitafanya Mkutano Mkuu Maalum kwa kuchagua viongozi watakaokiongoza chama hicho.

Moja ya nafasi hizo niya Mwenyekiti wa chama Taifa iliyoachwa wazi na Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad aliyefariki dunia Februari 17, 2021.

Nafasi nyingine niya Makamu Mwenyekiti pamoja na nafasi moja ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

Mgeni rasmi wa Mkutano huo ni Kiongozi wa chama kikuu cha Upinzani nchini Zimbabwe cha Citizen Coalition for Change (CCC), Ndugu Nelson Chamisa.

Ratiba ya mkutano huo wa kesho itaanza saa 2:00 asubuhi mpaka Saa 12:00 jioni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...