Na Denis Sinkonde, Songwe
Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Ilanga kata ya Mlale wilayani Ileje mkoani Songwe Subira Kibona(16) amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali mgongoni kisha kuchomwa moto na anayesadikika kuwa mme wake aliyefahamika kwa jina la Shukrani Kamwela (16) na mwili wake kutupwa kwenye kolongo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamada wa jeshi la polisi mkoani humo ASP Janeth Magomi amesema walipokea taarifa za tukio hilo juu ya mwanamke huyo ambaye alipotea nyumbani tangu januari 13 mwaka huu.
ASP Magomi amesema baada ya kutoonekana kwa marehemu huyo wananchi walifanya juhudi za kumtafuta na hatimaye kumkuta katika moja ya poli mwili wake ukiwa umechomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya mgongoni na kuchomwa moto huku ukiwa umetupwa kolongoni.
Hata hivyo ASP Magomi amesema chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na jeshi la polisi linaendelea kuchunguza na tayari mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi.
Diwani wa kata hiyo Yotamu Ndile amesema tukio hilo limetokea Januari 13 mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi baada ya mme wa marehemu kumwambia mke wake waende kwa mganga wa kienyeji kutafuta dawa tumbo maarufu kama kata kamba kwani marehemu alikuwa na ujauzito wa miezi saba.
Akizungumza na wananchi eneo la tukio afisa tarafa wa tarafa ya Bulambya Joyce Chale amewataka wananchi wa kijiji hicho kuwa na hofu ya Mungu kwani jamii inapaswa kutoa elimu kwa vijana namna ya kutatua migogoro inayojitokeza kwenye ndoa na si kukatisha uhai mtu ambaye ni gtegemezi kwa taifa.
Afisa huyo amewataka wananchi hao kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa za matukio kwani jeshi hilo linafanya kazi kwa kushirikiana na wananchi kwa lengo la kuwakamata waharifu na kuondoa dhana ya pindi wakitoa taarifa watakamatwa.
Aidha amewataka wazazi kuacha tabia ya kuwafanya watoto wa kike kama kitega uchumi bali wawapeleke shule ili kuepusha ndoa za utotoni.
Imeelezwa kuwa tukio hilo limekuwa la pili kutokea kijijini hapo la wanawake kuchomwa na kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa kuwa ni kisu huku wananchi wakiomba serikali kuchukua hatua za makusudi kuchukuia hatua kwa wahusika.
PICHA WANANCHI KATIKA POLI WALILOMKUTA MAREHEMU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...