***********************
Na Mwamvua Mwinyi Pwani
MSEMAJI Mkuu wa
Serikali , Gerson Msigwa amethibitisha Kuwa nchi haiwezi kuingia Gizani
kama baadhi ya watu wanavyodai ,kwani kinachofanyika ni maboresho na
matengenezo ya kawaida ikiwemo kituo Cha umeme wa gas Songosongo.
Aidha ameeleza,
hakuna mradi mikubwa ya kimkakati utakaokwama Wala uliokwama na yote
inaendelea vizuri huku wakandarasi wakiwa kazini.
Akizungumzia
utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya
sita,kwa waandishi wa habari Mkoani Pwani, Msigwa alisema, shirika la
umeme (TANESCO) linafanya maboresho ya kawaida na kuwepo kwa mgao ili
kuhakikisha upatikanaji wa umeme nchini unaongezeka.
“Watu waache kujaza
wengine maneno ya uzushi,kwani maboresho haya ni ya kawaida na nchi
haiwezi kuingia Gizani”alisisitiza Msigwa.
Msigwa
alisema kuwa kutokana na hali ya upungufu wa mvua umesababisha vyanzo
vya kuzalishia umeme maji kupungua hivyo kusababisha mgao ambao lengo ni
kufanya maboresho.
“Changamoto
hii ni kawaida hivyo wakati wa maboresho hayo yanayofanyika Songosongo
itasaidia hali kurejea kama kawaida na maboresho hayo hayatafanya nchi
kuingia gizani,” alisema Msigwa.
Alisema
kutokana na uboreshaji huo Watanzania wasiwe na hofu juu ya hali hiyo
kwani lengo la Tanesco ni kuhakikisha umeme unapatikana wa kutosha.
“Kuanzia
hiyo Februari Mosi ni kuboresha visima vya gesi vilivyopo Songosongo
hivyo wananchi waondoe hofu juu ya zoezi hilo,” alisema Msigwa.
Pamoja na hayo,
Msigwa alisema, ipo miradi mikubwa ya kimkakati Mkoa wa Pwani ikiwemo
Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere -Stigo lililopo Rufiji ambapo
ujenzi umefikia asilimia 55,Mradi mwingine ni reli ya kisasa (SGR )
uliofikia asilimia 95.
Alieleza kwamba,
Serikali inahakikisha miradi inaenda vizuri , na haijashindwa kuwalipa
wakandarasi na wakandarasi hao wanaendelea kulipwa.
Msigwa alifafanua hadi sasa Serikali imeshatoa fedha kwa wakandarasi na kazi inaendelea.
Kuhusu umeme alisema
kwa mkoa huo mradi wa REA II vijiji 89 vitafikiwa na kupitia mradi wa
Ujazilizi Bilioni 5.5 zimetengwa , Bilioni 12 pia imetumika na miradi
96 imeshakamilika.
Alieleza, Pato la mkoa limekua na kufikia Tirilioni 2.728 kwa mwaka 2019 .
Msigwa akizungumza
juu ya fedha za Uviko19 alibainisha, mkoa wa Pwani ulipelekewa Bilioni
16 , ujenzi wa madarasa 422,vituo shikizi vipya 37 na shule mpya za
Sekondari 11.
Fedha za elimu bila ya malipo imepelekwa Bilioni 5 na kusema Serikali inaendelea kuweka Mazingira bora kwenye sekta ya elimu.
Akizungumzia sekta ya
viwanda aliipongeza mkoa wa Pwani kwa kuwa ukanda wa viwanda,ambapo
hadi sasa una jumla ya viwanda 1,453 kati ya hivyo vikubwa 87, vya kati
177 na vidogo 1,057 na umetenga hekta 53.16 kwa ajili ya viwanda.
Upande wa dawa imefikia asilimia 89.5 na Serikali imeanzisha maduka ya dawa ili kurahisisha upatikanaji wa dawa.
Msigwa alikemea
Zahanati na vituo vya afya wilayani Kisarawe na maeneo mengine,
vinavyofungwa kabla ya wakati na kukemea watumishi wa afya wanaoshindwa
kutoa huduma bora kwa wananchi .
Akizungumzia barabara
ya Makofia-Mlandizi Msigwa alieleza, ipo Katika utekelezaji na Sasa
inafanyiwa upembuzi yakinifu hivyo wananchi wavute subira.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...