Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewahakikishia wananchi wa Kaskazini Pemba kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ataendelea kushirikiana na Rais wa Serekali ya mapinduzi ya zanzibar katika kuwaletea maendeleo Wananchi wa pemba na zanzibar kwa ujumla.

Katibu Mkuu ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa chama hicho katika maeneo tofauti Mkoa wa Kaskazini Pemba, Wilaya za Wete na Micheweni katika ziara maalum ya siku mbili akiambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya ccm Taifa.

Akitoa salam na ujumbe wa Viongozi Wakuu wa Serikali, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa wananchi wa wilaya ya Wete , Chongolo ameeleza kuwa;

"Rais Samia ameniambia niwahakikishie kuwa, ataendelea kushirikiana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi kupambana kwa ajili ya miradi na changamoto zinazowakabili ili ndani ya miaka mitano wilaya ya Wete na Pemba kwa ujumla kuwe na mabadiliko makubwa ya maendeleo."

Aidha, Chongolo ameeleza kuwa, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi amemtuma salaam zake kwao, awaeleze wananchi kuwa;

"Anajua changamoto ya maji iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa baadhi ya maeneo ya Wete, na amewahakikisha maji yatawafikia wananchi wote kama ilivyoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 - 2025 kama ilivyo kwa kijiji cha Taifu kilicho kuwa na uhaba wa maji kwa zaidi ya miKa 14 na sasa maji yanapatikana ya kutosha."

Aidha katika hatua nyingine Chongolo amewata wananchi wote kuwa macho kupita na kukagua miradi ya ujenzi wa hospitali za wilaya unaoendelea katika wilaya zote za Kaskazini Pemba ikiwemo Wilaya ya Wete ambapo zaidi ya shilingi bilioni 4 zimeshapelekwa na ujenzi unaendelea.

Aidha, Mbunge wa Jimbo Gando Salum Musa Omary ameishukuru chama na serikali kwa kuendelea kushusha fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo upatikanaji wa maji katika kijiji cha Taifu ambacho kilikuwa na uhaba kwa zaidi ya miaka 14.

Chongolo akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wete inayogharimu shilingi bilioni 4.71 amewataka vijana kuchangamkia fursa za mafunzo ya ufundi na ujuzi zinazotolewa na serikali ili kuweza kujipatia kipato kwa kushiriki ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa na hospitali unaoandela katika maeneo mbalimbali mkoa wa Kaskazini Pemba na Pemba nzima kwa ujumla.

Akizungumza na wanachama na wananchi kwenye kikao cha Mkutano wa Shina Namba 1, Tawi la Kiuyu, Kigongoni, Wilaya ya Wete, ametoa wito kwa wanachama wa CCM wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hiyo mwaka huu, lazima wajipime na wajue wajibu wa uongozi ndani ya chama ndani na nje ya chama, wasisukumwe na tamaa binafsi kutaka uongozi, bali kutumikia watu.

Pamoja na hayo, Chongolo katika maeneo tofuati mkoa wa Kaskazini Pemba amewataka wananchi kuhamasishana na kujiandaa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la sensa linalotarajiwa kufanyika mwaka huu, kwani takwimu ni msingi wa mipango ya maendeleo na usambazaji wa huduma za jamii.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mattar Zahoro Mattar amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, chini ya CCM, inayoongozwa na Rais Mwinyi imeamua kufanya Pemba kuwa mojawapo ya maeneo ya kimkakati kwa ajili ya uwekezaji kukuza Uchumi wa Buluu, kwa kuwapatia wawekezaji motisha kadri inavyowezekana kujenga mazingira rafiki.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...