Na Kassim Nyaki, UAE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi leo tarehe  17 Januari, 2022 ametembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya EXPO 2020 Dubai yanayoendelea katika Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu.

Mhe. Rais Mwinyi ambaye yupo katika ziara ya Kiserikali nchini humo ametembelea banda la Tanzania kwa ajili ya kjionea jinsi Tanzania inavyotumia fursa ya maonesho hayo ya Kitamaifa kujitangaza kupitia fursa mbalimbali za Utalii, Madini, Nishati, Kilimo na  fursa za uwekezaji kwa wageni wanaotembelea Banda hilo.

Katika ziara hiyo Mhe.Rais  amewapongeza watumishi wanaowakilisha Tanzania katika maonesho hayo kwa kuendelea kuitangaza Tanzania na fursa mbalimbali kupitia maonesho hayo.

Katika ziara hiyo Mhe. Rais Mwinyi ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb), Mhe. Balozi wa Tanzania katika Umoja nchi za Falme za Kiarabu Mhe. Mohammed Mtonga na Mke wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maryam Mwinyi.

Ujumbe wa Mhe. Rais umepokelewa na  Balozi wa Tanzania UAE Mhe. Mohammed Mtonga,  Mkurugezi wa Banda la Tanzania EXPO 2020 Dubai Bi. Getrude Gwashemi na Watumishi wa Taasisi mbalimbali za Serikali ya Tanzania walioko katika maonesho hayo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Bw. Rossan Mduma kutoka Bodi ya Utalii Tanzania alipokuwa akitoa maelezo jinsi Tanzania inavyotangaza vivutio vya Utalii wa wageni wanaotembelea banda la  Tanzania katika Maonesho ya dunia ya EXPO 2020 Dubai

Mke wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maryam Mwinyi (kulia) akiangalia madini mbalimbali ikiwemo Tanzanite alipotembelea banda la Tanzania katika maonesho ya EXPO 2020 Dubai

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa banda la Tanzania Bi. Getrude Gwashemi (kushoto) kuhusiana na mazao ya kimkakati ambayo ni moja ya fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi (kulia) akimsikiliza Bi. Latiffa Abdallah Kigoda (kushoto) kutoka TIC wakati akitoa maelezo kuhusu fursa za uwekezaji zilipo Tanzania pamoja na uboreshaji wa Miundombinu ya kimkakati inayotekelezwa Tanzania, katikati ni Balozi wa Tanzania UAE Mhe. Mohammed Mtonga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (wa nne kutoka kulia), Balozi wa Tanzania katika Nchi za Ummoja wa Falme za Kiarabu Mhe. Mohammed Mtonga (wa nne kutoka kushoto), wengine ni maafisa kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali ya Tanzania.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...