Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amesema Serikali inaendelea kujenga na kuboresha mazingira bora ya wawekezaji ili waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora na zitakazoweza kushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Kunenge amesema hayo leo Jumamosi Januari 29, 2022 akijibu changamoto zilizowasilishwa na baadhi ya wawekezaji wa viwanda wilayani Bagamoyo katika ziara yake ya kutembelea na kukagua shughuli zinazoendeshwa katika viwandani hivyo.
"Niwahakikishie wawekezaji endeleeni kuwekeza, umeme wa kutosha upo , na nasema hivi kwa sababu Rais wetu Samia Suluhu ametuahidi kuziondoa na ameanza kwa mradi huu wa Nyerere Hydropower Project huko Rufiji ambao umeme wake utazalishwa hapo na utatumika ukitokea hapa Chalinze inapojengwa mradi huo” amesema Kunenge
Kuhusu maji, mkuu huyo wa mkoa ameeleza Serikali imesaini mkataba na mkandarasi anafanya upembuzi yakinifu kutoa maji kutoka bwawa la mto Rufiji utakao zalisha lita milioni 250 kwa siku yatakayotumika Pwani na Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...