WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Wameshiriki  katika Wiki ya sheria kwa kuweka banda lao kwa ajili ya kutoa huduma.

Wiki hii ya sheria kwa kanda ya Dar  es Salaam inafanyika katika Mahakama ya hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam kuanzi Januari 23 hadi 29, 2022.

Huduma zinazotolewa katika banda la RITA katika wiki hii ya Sheria ni utoaji Elimu kuhusiana na  masuala ya kuandika na kuhifadhi wosia, huduma za usajili vyeti vya kuzaliwa na vifo, wanatoa elimu kuhusu masuala ya Mirathi na jinsi yanavyosimamiwa na ofisi ya RITA na masuala ya ndoa.

RITA wameshiriki katika wiki ya sheria kwa sababu ni wadau wakubwa wa sheria kila wanachokifanya kinahusiana na masuala ya sheria.

Wananchi wameaswa kutembelea katika banda la RITA kwaajili ya kujipatia huduma zinazotolewa pamoja na kujipatia Elimu.
Wananchi wakipata huduma katika banda la RITA ikiwa ni kuazimisha wiki ya sheria inayoendelea kufanyika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Salaam, kuanzia Januari 23 hadi 29, 2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...