Afisa Mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kitengo cha usubi ndani ya Wizara ya Afya, Oscar Kaitaba akizungumza wakati wa kuelezea kilele cha maadhimisho ya magonjwa hayo siku ya Jumapili mkoani Dodoma. Anayefuata ni Isaack Njau kutoka Kitengo cha Kichocho na Mohamed Nyati kutoka kitengo cha minyoo na tumbo.
Afisa Mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kitengo cha Kichocho, Isaack Njau akizungumza kuhusu kilele cha magonjwa hayo yatakayofanyika siku ya Jumapili mkoani Dodoma. Kulia ni Oscar Kaitaba wa Kitengo cha Usubi na kushoto ni Mohamed Nyati wa Kitengo cha minyoo na tumbo
Meneja wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipeumbele, Dk. George Kabona akizungumza kuhusu kilele cha maadhimisho ya wiki ya magonjwa hayo yatakayofanyika siku ya Jumapili viwanja vya Nyerere Square Dodoma. Wengine ni maafisa wa vitengo mbalimnbali kwenye mpango huo.
*Yapanga kuyatokomeza kufikia 2030
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha Maadhimisho ya Kimataifa ya siku ya magonjwa yaliyokuwa hayapewei kipaumbele.
Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ni pamoja na usubi, kichocho, minyoo ya tumbo, trakoma/vikope, matende na mabusha.
Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Taifa wa Kuratibu Magonjwa hayo Wizara ya Afya, Dk. George Kabona ameyasema hayo leo Januari 28, 2022 kuwa kilele cha maadhimisho hayo yaliyoanza tarehe 24 mwezi huu ni Jumapili tarehe 30 ambayo imetengwa kimataifa kuadhimisha magonjwa hayo.
Amesema maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila maka yatafanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square mkoani hapa na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali.
Amesema Tanzania ni miongoni mwa mataifa yaliyoathiriwa na magonjwa hayo na imekuwa ikitekeleza mpango wa kuyatokomeza hivyo kila mwaka hutenga wiki ya kuadhimisha magonjwa hayo.
Amesema lengo la siku hiyo ni kujikumbusha kwamba nchi inawajibu wa kutokomeza magonjwa hayo na kusherehekea mafanikio ambayo yamepatikana katika kuyadhibiti.
“Tunaangalia mafanikio kiasi gani tumepata na kujaribu kuondoa changamoto zilizopo kwa pamoja ili tuweze kufikia malengo kutokomeza magonjwa haya ifikapo mwaka 2030 ili yaondoke kabisa kwenye jami yetu,” alsiema
Amesema kuna magonjwa mengi nchini ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele lakini kuna matano ambayo yameathiri kwa sehemu kubwa ambayo kwa miaka 10 serikali imekuwa ikipambana nayo.
Amesema magonjwa hayo yako sehemu kubwa hapa nchini na yameathiri watanzania wengi na kichocho kimeonekana kuathiri zaidi watu wengi.
Amesema udhibiti wa magonjwa hayo ulianza miaka mingi iliyopita lakini mpango wa taifa wa kuyadhibiti kwa pamoja ulianza mwaka 2009 ambapo magonjwa hayo yaliunganishwa pamoja ili yadhibitiwe pamoja kwasababu yote yanafanana kwa kuathiri na madhara yake yanaonekana baada ya miaka mingi.
“Madhara yake si kiafya tu yanasababisha unyanyapaa kwa jamii na katika mifumo ya kutolea afya hayapewi kipaumbele kiasi kwamba mtu akipata magonjwa haya akienda hospitali si rahisi kupewa huduma,” amesema
Dk. Kabona amesema kupitia mpango huo ulioko Wizara ya Afya, Serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa kuhakikisha inahamasisha watu wayatambue na mifumo ya afya iimarishe huduma zake katika vituo vya kutoa huduma.
Amesema serikali imekuwa ikitoa elimu kupitia njia mbalimbali ili iweze kujikinga na magonjwa hayo ili watanzania wasipate madhara hayo ambayo huwa yanatokea taratibu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...