Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania imeendesha mafunzo ya wiki moja kwa taasisi tatu tofauti,wakiwemo wafanyakazi katika migodi, viwanja vya ndege, na Baraza la wawakilishi Zanzibar,ikiwa ni utekelezaji wa takwa ya kisheria, ambayo inaitaka Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania kutoa mafunzo kwa watumiaji wa vyanzo vya mionzi
Akizungumza Mkurugenzi mkuu wa Teknolojia na huduma za kiufundi TAEC,ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi mkuu Dkt.Remijius Ambross Kawala,aliwataka washiriki hao kutambua kuwa elimu waliyoipata juu ya usalama wa mionzi,itawasaidia kuwa watendaji bora na kuwajali wengine huku ikiwasaidia kuishi Maisha marefu,pamoja na kuisaidia jamii yao kuepukana na madhara yatokanayo na mionzi
Amewataka washiriki hao kuzichangamkia fursa zilizopo TAEC kwaajili ya kujali afya zao wawapo kazini,kutambua mazingira yao yenye viasili vya juu vya mionzi ,pamoja na kuhakikisha usalama na kuwalinda wengine bila kuvunja sheria ya nchi.
Amewasihi wale wote waliopata mafunzo kutoka sehemu za Mafia,Baraza la wawakilishi Zanzibar , machimbo ya madini Bulyanhulu,waweze kwenda kuwa mabalozi wazuri kwa kuwashirikisha wenzao ambao hawajapata mafunzo,sambamba na kuwatia moyo ili na wao waweze kupata mafunzo hayo
Mazoezi yako yoyote unayoyafanya sasa hivi lazima yajikite na kujali mazingira yaliyopo na haki ya mwenzako,kazi unayoifanya hakikisha haimuumizi mwenzako,Hatusemi ya kwamba teknolojia ya mionzi ina madhara kiasi hicho la hasha ,ila kitu chochote kina madhara kama utakiuka taratibu ya kukitumia ,mfano ndege ni nzuri sana lakini ikitokea hitilafu ni hatari,kila kitu chenye matumizi mazuri ukikiuka kinakuwa na matumizi mabaya.alisema Dkt.Kawala .
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo TAEC Dkt.Shovi Sawe alisema kuwa lengo la mafunzo hayo kwanza kabisa wanatekeleza matakwa ya kisheria ya nguvu za Atomiki Tanzania anmbayoinaitaka tume ya nguvu za atomiki Tanzania kutoa mafunzo kwa watumiaji wa vyanzo vya mionzi
Aidha alisemakuwa TAEC inataka kuwajengea uwezo waelewe namna salama ya kufanya kazi maeneo ya mionzi wao pamoja na wote wanaofanya kazi katika maeneo hayo ili waweze kuwa salama ,pamoja na mazingira ,na kuwaelekeza namana nzuri vyanzo vya mionzi vikishatumika au kuisha muda wake jambo gani wafanye ili waweze kuwa salama Zaidi
Na kwa utararibu tu ni kwamba watataikiwa vyanzo hivyo wavirudishe TAEC kwaajili ya uhifadhi wa store ya kutaifa au kurudisha kwenye nchi waliyotoa kwaajili ya kuhifadhiwa huko.
Akisisitiza utii wa sheria katika mionzi DKT.alisema mionzi ni moja vitu ambavyo vina manufaa makubwa kwa jamii na maendeleo ya kiuchumi lakini isipotumika vizuri ni mibaya sana,hivyo ndiyo sababau TAEC imekuwa ikikumbusha mara kwa mara hatua zichukuliwe ili kuhakikisha kuna usalama wa wafanyakazi,raia pamoja na usalama wa mazingira
Akifafanua mionzi kwa lugha rahisi Dkt.Shovi Sawe alisema nishati ambayo inatiririka kutoka vyanzo vya asili kama vile madini ya uranium,lakini pia ianweza ikawa ni nishati inayotiririka kutok kwenye vifaa vilivyotengenezwa na binadamu kama mashine za x-ray,ambapo binadamu ameweza kuona faida ya kuvitumia
Kwa upande wake mshiriki kutoka ofisi ya baraza la Utumishi Zanzibar Mohamed Bilal anasema hapo awali kabla ya kupata mafunzo walikuwa wanatumia mashine za kuskani lakini walikuwa hawafahamu usalama wao upo wapi ila kwa sasa baada ya mafunzo anajiona akiwa salama zaidi,ameahidi kwenda kuyatendea kazi kwa weledi yale yote aliyojifunza kwa faida yaw engine pia.
Amesema jamii inatakiwa kujifunza zidi kwani ipo tabia ya kuchukua vitu ambavyo vimeshatumika ambavyo havifahamiki usalama wake zaidi,hivyo ameishauri jamii kutokupenda kutumia vitu ambavyo vimeshapitwa na wakati, kwani ni hatari kwa afya zao,badala yake wachukue vitu vipya ili waweze kuwa salama Zaidi.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya walioshiriki mafunzo mwenyekiti wa muda amewashukuru TAEC kwa mafunzo hayo,kwani wameongeza vitu vingi ambavyo hapo awali walikuwa hawavitambui ,na ameahidi kwenda kuwa mabalozi wazuri ,na kuaahidi kuzingatia na kuyapa kipaumbele ,huku wakifuata taratibu zote za kiusalama mionzi ni mizuri.
Washiriki 19 kati yao 5 wametoka Baraza la wawakilishi Zanzibar 1 kutoka kiwanja cha ndege cha Mafya na 12 kutoka mgodi wa Bulyanhulu kahama ambapo hadi sasa tangia kuanza kwa robo mbili zilizopita wameshiriki 303 julai-dec 2021 alisema Dkt.Shovi Sawe.

Dkt.Shovi Sawe Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo TAEC:ni kawaida yetu kufanya mafunzo vya mionzi ambapo 17/21/2022 tumeanza kutoa kwa wafanyakazi ikiwa ni kutekele matakwa ya kisheria ya nguvu za Atomiki Tanzania ambayo inaitaka tume ya nguvu za atomiki Tanzania kutoa mafunzo kwa watumiaji wa vyanzo vya mionzi
Mkurugenzi mkuu wa Teknolojia na huduma za kiufundi TAEC,ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi mkuu Dkt.Remijius Ambross Kawala akizungumza na washiriki wa mafunzo ya wiki moja juu ya kupata elimu juu ya usalama wa mionzi katika kufunga mafunzo ya wiki moja yaliyofanyika makao makuu ya TAEC mkoani Arusha.
Mkurugenzi mkuu wa Teknolojia na huduma za kiufundi TAEC,ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi mkuu Dkt.Remijius Ambross Kawala akumkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo juu ya usalama wa mionzi mmoja wa washiriki kama inavyoonekana katika picha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...