Na John Walter-Manyara
Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) Mkoa wa Manyara, Mhandisi Hamisi Rahisi amesema wamedhamiria
kuondoa kero ya kushindwa kuwafungia umeme wateja wake kwa wakati.
Ameeleza
kuwa hatma ya wateja wenye namba ya malipo ya bei ya shilingi
27,000,wafike ofisi za TANESCO kwa ajili kupata namba mpya za malipo.
Mhandisi
Rahisi amesema hayo Jumatatu Januari 20, 2022 wakati akitoa ufafanuzi
kuhusu gharama za kuunganisha huduma ya umeme kwa wananchi wa mkoa wa
Manyara, ambapo amesema katika maeneo ya vijijini wataendelea kulipia
Sh27, 000 kama kawaida na maeneo ya mjini na miji wataunganishiwa kwa
gharama mpya.
Amesema mpango huo wa kuwaungishia umeme wananchi hao ambao walikuwa wamelipia Shilingi 27, 000 utaendelea.
Mhandisi
Rahisi amesema Tanesco imeanza kutumia bei mpya za kuunganisha umeme
Januari 5 mwaka huu huku ikisema Sh 27,000 itatumika kwenye maeneo ya
vijiji pekee.
Amesema maeneo yatakayolipia gharama halisi za
kuunganisha umeme kwa umeme wa njia moja ndani ya umbali wa mita 30
kutoka kwenye miundombinu ya umeme ni shilingi 320,960, kwa mteja wa
njia moja ndani ya umbali wa mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme
ni shilingi 515,618.
Kwa mteja wa njia moja ndani ya umbali wa mita
120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme ni shilingi 696,670, njia tatu
ndani ya umbali wa mita 30 kutoka kwenye miundombinu ya umeme ni
shilingi 912,014.
Ameongeza kuwa kwa mteja wa njia tatu ndani ya umbali wa mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme ni shilingi 1,639,156.
Kwa
upande wa vijijini amesisitiza kuwa kwa njia moja gharama ni shilingi
27,000 na kwamba kikosi maalum kinashughulikia maombi ya zamani
yakamilike.
Amesema Chanzo cha bei hizo ni kwa mujibu wa mamlaka ya
udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA) ambapo gharama halisi
ziliidhinishwa Novemba 25,2020 baada ya kupitia mchakato wa tathmini ya
bei kulingana na gharama halisi ya vifaa vya uunganishaji umeme pamoja
na uendeshaji.
Kwa upande wake afisa Uhusiano wa TANESCO mkoa wa
Manyara Marcia Simfukwe amesema katika maeneo ya Halmashauri ya mji wa
Babati yenye kata nane yapo maeneo ambayo yanahesabika vijiji kwa mujibu
wa TAMISEMI hivyo yataendelea kuunganishiwa umeme kwa gharama ya
shilingi elfu 27,000.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...