Katibu Mkuu, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara (Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele Mene walipokutana pamoja na kufanya mazungumzo Januari 24, 2022 katika Ofisi za Makao Makuu ya Sekretarieti hiyo yaliyopo Accra, nchini Ghana.



KATIBU Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika AfCFTA, Sekta Binafsi na Wadau wengine nchini kuwaelimisha wananchi kuchangamkia fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana katika Eneo  hilo. 

Katibu Mkuu ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na  Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya AfCFTA 

Mhe. Wamkele Mene Januari 24, 2022 katika Ofisi za Makao Makuu ya Sekretarieti hiyo yaliyopo Accra, nchini Ghana. 

Pamoja na mambo mengine yaliyojiri katika mazungumzo hayo, Prof. Kahyarara alimpongeza Mhe. Wamkele kwa hatua nzuri iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mkataba wa AfCFTA na kusisitiza utayari wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kushiriki kikamilifu katika kutekeleza Mkataba huo. 

Naye Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya AfCFTA Mhe. Wamkele Mene aliipongeza Tanzania kwa kuwasilisha Hati ya kuridhia mkataba wa AfCFTA kwenye Kamisheni ya Umoja wa Afrika na kuwa nchi ya 40 kati ya nchi 55 za Afrika kufanya hivyo na alitoa wito kwa Watanzania wenye vigezo stahiki kuchangamkia fursa za kazi zinazoendelea kutangazwa na Sekretarieti ya AfCFTA. 

Aidha , Viongozi hao walikubaliana kuendelea kushirikiana katika masuala yanayohusu Mtangamano wa Afrika kupitia Mkataba wa AfCFTA hususani katika kukuza uwekezaji katika Sekta ya Usafirishaji na Uwezeshaji Biashara, Uongezaji thamani mazao ya kilimo na  uzalishaji madawa 

Katibu Mkuu, Prof. Godius Kahyarara yupo nchini Ghana kushiriki Mkutano wa 10 wa Maafisa Waandamizi wa Biashara wa Afrika unaofanyika Accra, Ghana kuanzia tarehe 24-27 Januari 2022. Mkutano huo utafuatiwa na Mkutano wa Nane (8) wa Baraza la Mawaziri wa Biashara wa Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 28-29 Januari 2022. 

Prof. Godius Kahyarara, Katibu Mkuu, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara (Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Wamkele Mene, Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...