Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma kuhusu kukamilika kwa zoezi la uteuzi na utaratibu wa Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Katibu wa Bunge hadi kufikia leo saa Kumi Jioni Majina ya jumla ya Wagombea Tisa (9) yalikuwa yamewasilishwa na kukidhi matakwa ya kisheria kwa ajili ya uchaguzi wa Spika unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 1 Februari, 2022.

Aidha, Katibu wa Bunge amesema miongoni mwa Wagombea hao nane sio Wabunge na mmoja ni Mbunge. Aliwataja magombea hao kuwa ni Abdulla Mohammed Said (NRA), Mhandisi Aivan Jackson Maganza (TLP), David Daud Mwaijolele (CCK), George Gabriel Bussungu (ADA -TEA), Kunje Ngombale Mwiru (SAU), Maimuna Said Kassim (ADC), Ndonge Said Ndonge (AAFP), Saidoun Abrahaman Khatib (DP) na Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...