WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Januari 16, 2022 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ikulu inayojengwa katika eneo la Chamwino, Jijini Dodoma na kusema ameridhishwa na kasi ya ujenzi na ubora wa majengo hayo na amemtaka mkandarasi ahakikishe mradi huo unakamilika mwezi mei mwaka huu.

 

Waziri Mkuu amewasisitiza wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kwa wakati na kuwapongeza wote wanaohusika na ujenzi. “Tunataka kumuwezesha Mheshimiwa Rais kufanya kazi katika eneo lake maalum na afanye kazi katika mazingira mazuri na kwa ufanisi.”

 

“Nimefurahishwa na taarifa kwamba ujenzi huu umefikia asilimia 91 na hatua iliyobaki hizi asilimia 9 ni kazi ndogondogo kama uwekaji wa milango, njia za mifumo ya hewa na umeme na zote zinaenda vizuri.” Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan pia anatarajia kuona ujenzi huo unakamilika kwa wakati.

 

Waziri Mkuu amelipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kutekeleza ujenzi huo kwa ufanisi. “Ramani iliyoko hapa iko sawasawa na jengo la Ikulu lililoko Dar es Salaam, Wakandarasi wetu mmefanya kazi kubwa sana, Hii imedhihirisha kuwa nchi yetu ina wataalam wa kutosha kujenga aina yoyote ya majengo.”

 

Kwa Upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mhandisi Daudi Kondoro amemhakikishia Mheshimiwa Waziri Mkuu kwamba mradi huo utakamilika na kukabidhiwa mwezi Mei kama inavyotarajiwa kwani sasa uko katika hatua za mwisho za ukamilishaji.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Ikulu), Dkt. Mosses. Kusiruka (wa tatu kulia), Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja General Rajabu Mabele (wa pili kulia) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Daudi Kandoro (kulia). Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, Januari 16, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma,  Januari 16, 2022.  Kushoto  kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Mosses Kusiruka na kulia kwake ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali, Rajabu Mabele. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mhandisi Daudi Kondoro (kulia) ambaye alitoa maelezo mafupi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Ikulu   ya Chamwino jijini Dodoma, wakati Waziri Mkuu alipokagua ujenzi huo, Januari 16, 2022. 

Muonekano wa  Jengo la Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma linalojengwa na SUMA JKT ambalo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake, Januari 16, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...