Mdau wa Maendeleo wa Ulanga Nicolus Mpandula akizungumza na waandishi wa habari juu ya mbunge wao kuvunjiwa heshima na baadhi ya wananchi wakidai amedhurumu jiwe na shilingi milioni mbili.
Mdau wa Maendeleo wa Ulanga Nicolus Mpandula  akiwa na waandishi wa habari.

*Ni Mbunge Salim Almas ahusishwa madai ya uongo

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
WADAU Wa Maendeleo Mkoa wa Morogoro wilaya ya ulanga wametaka baadhi ya watu Jimbo la Ulanga kuacha majungu ya kisiasa dhidi ya Mbunge wa Jimbo hilo Salim Hashim Almas.

Wadau wamejitokeza baada ya kuona Mbunge anafedheshwa juu ya kuwazulumu wenzie jiwe na sh.milioni mbili ambapo wanaamini hana ujasiri huo wa kufanya hivyo kutokana na kufadhili miradi mbalimbali ya mamilioni.

Akizungumza na Waandishi Wahabari Mdau wa Maendeleo katika Jimbo la ulanga,   Nicolaus Mpandula amesema kutokana na juhudi nyingi anazofanya Mbunge huyo ni wazi kuwa lipo kundi la watu wenye chuki nae na kuzusha Maneno yenye mlengo wa kumchafua Mbunge huyo na hivi karibuni imezuka taarifa na kusemekana kuwa Mbunge huyo amehusika kudhulumu jiwe la Madini lenye thamani ya shilingi milioni mbili.

"Huku ni kumkosea adabu na kumvunjia heshima kiongozi wetu, kwani mambo anayofanya kabla ya kuwa Mbunge na hata baada ya uongozi alipo Kwa Sasa hakuna Mwana ulanga asiyefahamu upendo wa Mbunge huyu ambapo Kwa wakati wote amekua mtu wa kujitolea katika jamii Kwa mfuko wake binafsi."

Aidha, Mpunda amebainisha Maendeleo ambayo Mbunge huyo ameyafanya Kwa jamii yake katika harakati za kuleta Mabadiliko na Maendeleo katika Jimbo la ulanga Mkoa wa Morogoro.

"Amechangia Mifuko 100 ya Saruji Kwa ajili ya ujenzi wa Shule za Kata na Shule shikizi za Msingi na Sekondari Kila kata,amenunua gari Maalum Kwa ajili ya kuchimba kisima katika kituo cha Afya Mwaya Ili kuboresha upatikanaji wa Maji safi na salama kirahisi na kuwapunguzia adha wakina Mama waliokua wakitembea umbali mrefu kutafuta Maji."

Hata hivyo Mpandula amefafanua zaidia juhudi zingine ambazo amekwisha zifanya Mbunge huyo amefanya juhudi mbalimbali katika Jimbo ikiwemo kuchangia Fedha kiasi cha shilingi milioni 10 Kwa ajili ya kuboresha nyumba ya kuhifadhi Maiti.

Pia amewataka Wananchi wajimbo la Ulanga kupuuzia shutuma hizo kwani hazina ukweli wowote ule.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...