Na Said Mwishehe, Michuzi TV
MAKADA saba wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) wamejitosa hadi muda huu kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo.

Hatua hiyo inakuja siku moja tu baada ya CCM kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka kutanza kuanza kwa mchakato wa kumtafuta Spika wa Bunge kufuatia kujiuzulu kwa Job Ndugai aliyekuwa katika nafasi hiyo

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika ambazo Michuzi TV na Michuzi Blog imezipata zinaeleza kuwa waliojiochukua fomu ya kuwania nafasi hiyo nyeti ni Naibu Spika Dk.Tulia Ackson,aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi,aliyekuwa Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi.

Wengine ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu, Kihenzile, Adv Ukashu pamoja na Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.Hata hivyo mchakato wa uchukuaji fomu kwa ajili ya kuwania nafsi hiyo umeanza leo Januari 10 na litamalizika Januari 15, hivyo kunatarajiwa wengi zaidi watajitokeza

Kwa mujibu wa ratiba ya CCM, baada ya kukamilika kwa mchakato wa uchukuaji fomu zakuwania U-Spika kuanzia Januari 18 hadi Januari 19 kutakuwa na kazi ya kuchuja majina na kisha kufanya uteuzi wa mwisho.Kazi hiyo itafanywa na Kamati Kuu.

Kuanzia Januari 21 hadi Januari 30 mwaka huu 'Cocus' ya Chama ya wabunge wa CCM itapiga kura kumpata mgombea ambaye atakwenda Bungeni kuomba kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo wakati mchakato huo ukiwa umeanza tayari kunaonekana kuwepo kwa vita ya chini chini kati ya wagombea hao ambapo kila mmoja anasuka mikakati itakayomuwezesha kuwa Spika.

Michuzi Blog na Michuzi TV itaendelea kukupa kila aina ya taarifa kuhusu yanayoendelea katika wakati wote wa kumpata Spika wa Bunge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...