TAARIA zinazozagaa kwa sasa ni kuwa Kampuni ya simu za mkononi ya itel inatarajia kuachia simu kali inayotajwa kuwa ni ya kundi la ‘A ‘series yaani A58 itakayokata kiu ya watumiaji wa smartphone.
Taarifa zilizovuja ni kwamba simu ina skrini yenye ukubwa wa inchi 6.6” HD Full Screen, huku ikisifiwa kwa kuwa na betri inayodumu zaidi na chaji ambapo imekaririwa kuwa ina 4000mAh.
Muundo wake unasemekana kuwa ni mzuri na wenye
kuvutia hasa kwenye kingo zake, simu hii inatarajiwa kuteka soko la smartphone
hasa kwenye suala la bei ambapo inasemekana kuwa itauzwa kwa bei nafuu sana.
Mwonekano
wa kingo za itel itel A58
Aidha itel
imeanzisha mfumo wa mtandaoni unaojulikana kama egatee utakaowawezesha wafanyabiashara yaani wenye maduka ya
simu kununua au kuweka oda ya simu na
bidhaa nyingine moja kwa moja na kisha kuletewa bidhaa hizo kwenye maduka
yao. Tayari zaidi ya wafanyabiashara
5,000 wameshajiunga na mfumo huo kwa kupakua App hiyo ya egatee.
Inaelezwa kuwa faida ya mfumo huo kwa wenye maduka ya simu na wauzaji kwa ujumla ni pamoja na kuokoa muda, kufaidi punguzo la bei, kupewa zawadi mbalimbali mara tu baada ya kununua bidhaa zake kwenye mtandao huu na vilevile kupata ofa mbalimbali za siku, wiki na mwezi.
Je, ungependa kufahamu zaidi kuhusu ujio wa simu hii itel A58? Tafadhali tembelea ukurasa wao wa Facebook itel Tanzania au Instagram bofya link: https://www.instagram.com/iteltanzania/
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...