Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam( DIT) Profesa Preksedis Ndomba(wa pili kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda(katikati) baada ya kufanya ziara ya kikazi kwenye taasisi hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amepata nafasi ya kushudia ubunifu na uvumbuzi uliofanywa na DIT.


Na Said Mwishehe, Michuzi TV 

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema umefika wakati kama nchi kuanza kuweka mkakati ambao utawezesha kuanza kutengenezwa kwa vipuri vya aina mbalimbali vikiwemo vya bajaji na magari ili kuondokana na uagiza vipuri nje ya nchi.

Profesa Mkenda ametoa kauli hiyo leo Januari 28, 2022 aakiwa katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ambapo amefika kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzunumza na menejimenti sambamba na kushuhudia bunifu mbalimbali za sayansi na teknoloji zilizofanywa na wanafunzi waliosoma na wanaondelea kusoma katika taasisi hiyo.

"Nimefurahishwa sana na uvumbuzi na ubunifu unaofanyika hapa DIT na sasa uwe wa kibiashara na kuanza kuzalisha kwa bidii zaidi, tunachohitaji ni sisi kuwapa nguvu zaidi ya  kuzalisha si hizi bidhaa za matumizi ya kawaida.Tunataka  bidhaa za aina ya vipuri , tunayo  magari chungu mzima hapa nchini lakini tunanunua vipuri kutoka nje.

"Hizi pikipiki ambazo vijana wanaendesha kila siku lakini tunanunua vipuri kila siku , vipuri hivi vinahitajika sana, hivyo kampuni hii tanzu inaweza kuviangalia na kisha tukaanza kutengeneza vipuri vyetu.Tunahitaji kuanza kuzalisha baadhi ya vitu vidogo tu kama bajaji , kama tutaweza kuzalisha kitu kama hicho hata kama Injini tutakuwa tunaagiza kutoka nje hapo tutakuwa tumeanza katika safari ya sayansi na teknolojia.

"Tunaambiwa hata Mbuyu ulianza kama mchicha,ukiangalia nchi kama India walipoanza kuzalisha Tata watu waliwacheka lakini sasa hivi wamekuwa wakubwa, South Korea hivyo hivyo, Japan hivyo hivyo na sisi hatutali na hatuwezi kupita barabara tofauti na wenzetu waliyokwenda,"amesema.

Amefafanua kwa hiyo amefurahi kuona aina ya uvumbuzi na ubunifu ambao umefanywa na Taasisi ya Teknolojia,na baada ya kufanya mazungumzo na menejimenti atakuwa akizitembelea mara kwa mara taasisi za sayansi na teknolojia pamoja na vyuo vya ufundi.

"Wakati tunaimarisha ubora wa elimu ya juu, ubora wa elimu ya msingi na sekondari tunataka vyuo vyetu vya ufundi kama hiki cha DIT na VETA viwe ninasaidia zaidi kuliko wanavyofanya sasa hivi, moja ni uwajibikaji wa vijana wetu na kujiajiri kwa vijana wetu.DIT watusaidie katika mabadiliko ya teknolojia.

"Kitu kinachozalishwa Uturuki tunakileta hapa , tuangalie uwezo wa kubadilisha ujuzi kutoka mataifa mengine na kisha tunauleta nchini kwetu, tunazalisha bidhaa na kuuza ndani ya nchi na nje ya nchi, kwa mfano sasa hivi tukiweza kuzalisha vipuri vya bajaji na tukaona vinafanya vizuri basi tutakwenda Hazina kuomba waongeze kodi kwa vile vinavyotoka nje ili kuongeza uzalishaji wa ndani.

"Na baadae Tanzania ikawa mzalishaji mkubwa wa vipuri hivyo.Tunahitaji kupiga hatua katika eneo la sayansi na teknolojia kama Ilani ya CCM inavyoelekeza , kwa mfano wale vijana ambao tunawaaajiri kama wakufunzi tunawapeleka nje kusoma.

"Nimefurahi  kukuta Mkuu wa Taasisi ya DIT anajenga mahusiano na vyuo vikubwa vya nje ya nchi ambavyo vinasifika duniani katika eneo la sayansi na teknolojia.hivyo vijana wetu wakimaliza Shahada za Uhandisi na wakafanya vizuri  sana tuwasomeshe sisi kama Serikali,"amesisitiza.

Profesa Mkenda amesema wana mpango mwingine wa kuhakikisha wanafanya mkutano na watanzania ambao wamebobea katika ujuzi na wanafundisha vyuo vikubwa vya sayansi na teknolojia huko nje."Tukae nao na tuone namna gani tunaweza kushirikiana kukuza sayansi na teknolojia nchini kwetu , watuambie ni namna gani wanaweza kutusaidia kupeleka vijana wetu kusoma katika vyuo hivyo.

"Huwezi  kufunga mipaka ya teknolojia , lazima tuangalie wenzetu wanafanya nini , wanasema kwa sasa huna haja ya kugudua tairi maana lilishagunduliwa unachotakiwa kufanya ni kuboresha kile ambacho kimegunduliwa, twende huko walikogundua na vijana wakija hapa watakuja kuboresha na tutakwenda mbele zaidi,"amesema Profesa Mkenda.

Mhitimu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) Joan Mohamed (aliyekaa) akitoa maelezo kwa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda kuhusu ugunduzi wa kiti cha walemavu ambacho amekibuni kwa ajili ya kusawasaidia watu wenye ulemavu na walipooza mwili ili waweze kufanya shughuli zao kama wengine.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda (katikati) akifafanua jambo kwa viongozi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) baada ya kufanya ziara ya kikazi katika taasisi hiyo leo Januari 28,2022.
Profesa Adolf Mkenda (katikati)ambaye ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia akiangalia kiti cha walemavu ambacho amekibuni mmoja wa wahitimu wa Taasisi ya DIT Joan Mohamed (aliyesimama kushoto)







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...