Na. John Mapepele, WUSM

 WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kassim Majaliwa Majaliwa leo Januari 27, 2022 ametoa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati -Cornell ya Fasihi ya Afrika  kwa washindi wa mwaka 2021 jijini Dar es Salaam. 

Katika kundi la Riwaya Halfani Sudy ameibuka kuwa mshindi wa kwanza, Mohamed Omary ameibuka mshindi wa kwanza kundi la shairi, wakati Mbwana  Kidato ameibuka mshindi wa pili katika kundi la tamthilia  na Lukas Lubungo kuwa mshindi wa pili  kwenye kundi la hadithi za kubuni.

 Amesema dhamira ya Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ya kutekeleza mkakati wa kubidhaisha lugha ya Kiswahili Kitaifa na Kimataifa, ambao utazinduliwa hivi karibuni itafanikiwa ikiwa wadau wote watajitoa kwa dhati kutekeleza mkakati huu na kusimamia maendeleo ya lugha hii adhimu na aushi. 

Mhe. Majaliwa amezipongeza kampuni za SAFAL na ALAF kwa kufadhili tukio hilo na  ametoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano huo kwa kuwekeza katika lugha hiyo, huku akisisita kuwa kuwekeza katika Kiswahili itakuwa ni njia mojawapo ya kurudisha fadhila kwa wananchi ambao ndio wateja wa bidhaa hiyo.

 Aidha,  Mhe Majaliwa amesema Kiswahili kimetambuliwa kimataifa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)  na kutangaza tarehe 7 mwezi Julai, kila mwaka kuwa Siku ya Kiswahili Duniani ambapo ameitaka  Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuanza kuandaa wiki ya maadhimisho ya kiswahili katika  siku ya mwaka huu. 

 Naye, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Wizara yake itashirikiana na wadau mbalimbali kukuza lugha ya kiswahili ili kufika sehemu mbalimbali duniani.

Mhe. Mchengerwa  ameelekeza wadau mbalimbali wa lugha ya  hiyo kuhakikisha wanaisherekea  kwa namna ya pekee siku ya kiswahili ya Julai 7 mwaka huu kwa namna ya kipekee ili kuthibitishia dunia kuwa  Tanzania ndiyo chimbuko la lugha hiyo.

 Katika  halfa hiyo,  Waziri Mkuu  Mhe Majaliwa na Mhe. Mchengerwa walitumia nafasi hiyo kumtakia heri ya kuzaliwa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa wimbo wa kiswahili wa heri ya kuzaliwa uliongozwa na Jaji Mkuu wa tuzo hizo Profesa  Aldin Mutembei kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salam.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...