Leo jioni nikiwa natokea Kijiji cha Kwa Lukonge,Tarafa ya Mombo Wilayani Korogwe nilipata nafasi kusimama kwa Mzee Athumani Juma maarufu kama “Mvumbuzi” ambaye anatengeneza Korona (mashine ya kuchakata mkonge) kwa usaidizi wa wake zake wanne.
Moja kati ya changamoto kubwa kwa wakulima wa mkonge ni upatikanaji wa Korona,Mzee Mvumbuzi aliiona fursa na sasa anazitengeneza nyumbani kwake.
Mh Waziri Mkuu Kassim M. Majaliwa alimtembelea katika karakana yake na kutoa maelekezo ya Mzee Mvumbuzi kuunganishwa na CARMATEC,SIDO,VETA na BRELA(kulinda ubunifu wake)sambamba na Bodi ya Mkonge Tanzania kumtafutia masoko ya mashine zake na ambapo kwasasa amefanikiwa kuliteka soko la ndani na nje ya nchi huku akiwa anauza mashine zake nyingi nchini Kenya.
Nimefurahishwa na ubunifu wa Mzee Mvumbuzi na kwa nafasi yangu;
1.Nimewaelekeza Bodi ya Mkonge kumsaidia kumtafutafutia mtaalamu wa kumuandikia andiko la biashara ili kupata fedha za kuongeza mtaji wa biashara yake kupitia Mifuko ya Uwezeshwaji na Taasisi za Fedha.
2.Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ione namna nzuri ya kuwakopesha vijana mashine hizo kwenye mikopo ya **4% **ya mapato ya ndani ili kiwe chanzo cha kipato kwa Vijana na kumuongezea soko la mashine zake Mzee Mvumbuzi.
3.Halmashauri kumtafutia eneo kubwa zaidi la Karakana ili kuongeza wigo wa uzalishaji mashine nyingine zaidi na kupata nafasi ya kurithisha ujuzi kwa watu wengi zaidi.
Creativity is thinking up new things,Innovation is doing new things.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...