Na WAF - Makete, NJOMBE.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel leo amekabidhi vifaatiba kwa ajili ya huduma za matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Makete.

Dkt. Mollel amekabidhi vifaatiba vyenye thamani ya Shilingi Milioni 15 ambavyo vimetolewa na Mfuko wa Doris Mollel wakishirikiana na Segal Family Foundation ili kusaidia watoto njiti wanaozaliwa na akina mama katika Hospitali ya Wilaya ya Makete wanatunzwa vyema na kuwa na afya bora.

Dkt. Mollel ameipongeza Taasisi ya Doris Mollel inayoongozwa na Bi.Doris Mollel kwa kuendelea kusaidia jamii ya Watanzania katika masuala ya uzazi na kuwataka Watanzania wengine na Taasisi mbalimbali nchini kuwa Wazalendo na kujitoa kusaidia jamii.

Awali akizungumza Bi. Doris Mollel amesema kuwa Taasisi yake imekuwa ikijishughulisha na kusaidia Huduma za Uzazi na matunzo ya Watoto Njiti na tayari wamekwishazunguka maeneo mbali mbali nchini na kufanya kazi na Wilaya zaidi ya 45.

"Leo tumekuja hapa Makete kuleta mashine hizi 3 za kufua oksijeni kwa ajili ya watoto njiti, mashine hizi zinauwezo wa kuhudumia watoto sita kwa wakati mmoja" amefafanua Bi. Doris Mollel

Katika tukio lingine Dkt. Mollel amekabidhi vifaatiba vya maabara, Jokofu la kutuza maiti 4 kwa wakati mmoja pamoja na mashine ya kufulia nguo ambavyo vimenuniliwa na Serikali kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Makete.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Makete Mhe. Festo Sanga ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuboresha huduma za afya katika Wilaya ya Makete.

"Mashine hizi zilizotolewa leo tunaamini zitakwenda kutusaidia sisi wanamakete kuboresha huduma za afya na kuwapunguzia kero hawa wananchi" amesema Mhe. Sanga

Mhe. Sanga ameupongeza Mfuko wa Doris Mollel kwa kufika Makete na kutoa msaada katika Hospitali ya Makete ambayo ilikuwa na uhitaji wa vifaatiba kwa ajili ya kusaidia watoto njiti kuweza kupumua vizuri.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akikata utepe mara baada ya kupokea mashine 3 za kufua hewa ya Oksijeni kutoka Doris Mollel Foundation zenye thamani ya Shilingi Milioni 15 zilizotolewa katika Hospitali ya Wilaya ya Makete

 Mashine za kufua hewa ya Oksijeni zilizotolewa na Doris Molle Foundation leo kwa ajili ya kusaida watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya ya Makete

Naibu Waziri wa aafya Dkt. Godwin Mollel akiangalia khanga zilizotolewa kwa wazazi walio katika Hospitali ya Wilaya ya Makete, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Doris Mollel Foundation Bi. Doris Mollel
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel pamoja na Bi. Doris Mollel Mkurugenzi Mtendani Mfuko wa Doris Mollel wakikabidhi zawadi ya Khanga kwa mzazi aliyejifungua mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Makete

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akisalimiana na wananchi waliofika katika Hospitali ya Wilaya ya Makete kwajili ya huduma za matibabu.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Molle (katikati) akifurahi mara baada ya kukabidhi vifaatiba vya maabara vilivyotolewa na Serikali kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Makete



Mkurugenzi Mtendaji wa 'Doris Mollel Foundation' Bi. Doris Mollel akisema jambo wakati wa hafla ya makabidhiano ya mashine 3 za kufua hewa ya Oksijeni kwa ajili ya kusaidia huduma za tiba wa watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya ya Makete.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...