Adeladius Makwega,DODOMA.

Wakaazi wa kata ya Ketaketa, Wilaya Ulanga, Mkoani Morogoro wamesema kuwa tangu kuvunjika kwa daraja shikizi Februari mosi 2022 wameanza kulipishwa fedha ya kuvushwa kutoka upande mmoja na kwenda upande wa pili wa daraja hilo linalounganisha Vijiji cha Ikangao na Ketaketa katika kata hiyo inayopakana na Mbuga wa Selouu na Mkoa wa Lindi

Wakizungumza kutokea vijiji hivyo kwa njia ya simu, Katibu wa CCM wa Kata hiyo Ndugu Merdad Saada alisema kuwa ni kweli daraja limebomoka na hivi sasa mwendo unaendelea ni wa mwendo pesa vuka, pesa rudi, malipo.

“Hamna chochote, hatuna hata cha kuzungumza, shilingi 500 kwa baiskeli, kwa mguu shilingi 200 na bodaboda ni shilingi 1000.”

Katibu wa huyo wa CCM alisema kuwa katika kata hiyo karibu robo tatu ya wakaazi wake ndiyo walioathirika zaidi kwa kubomoka kwa daraja hilo, huku robo ni wakaazi wa Luhombero Misheni eneo linakaribiana na kata ya Ilonga (Chigandugandu)

Kwa upande wake Pankras Pankras Mtemike ambaye ni mwenyekti wa Umoja wa Vijana wa CCM kata hii amesema kuwa ameshuhudia kwa macho yake wananchi wakilipishwa kiasi hivyo vya fedha na vijana waliojipatia ajira.

“Ukiwa wewe na pikipiki yako kuvushwa kule ng’ambo unatakiwa kutoa shilingi 1000, wewe 500 na pikipiki yako 500 na kurudi hivyo hivyo wewe 500 na pikipiki 500, ukiwa wewe na baiskeli yako ni 500 na hiyo ndiyo biashara inayoendelea sasa hivi.”

Pia amedai kuwa kuwa hata robo ya watu hao wa Luhombero Misheni wanayo mashamba yao upande wa pili wa daraja hilo Je wanafikaje huko ikiwa sasa ni msimu wa kilimo?

“Sasa hivi tunapambana na hali ya mvua tu, mvua inashuka, tunapanda mazao, maeneo ya bondeni maji yanapita kwa spidi yanahamisha mpaka mbegu zenyewe, inabaki ardhi peke yake, tunaanza tena upya, hii ndiyo changamoto tuliyonayo. Inasomba kila kitu kwa kuwa tumelima kwa matrekta, kwa hiyo udongo unasombwa pale, unakuta ardhi yako yako ya msitu udongo unakwenda kwa jirani yako. Kwa mfano ufuta kwa sababu umeshaanza kuota mvua ikija unafukulika, unakwenda na maji, mvua huku kwetu imezidi.”

Kiongozi huyo wa CCM wa kata hiyo pia aliongeza kuwa japokuwa mvua hii inayonyesha ina madhara makubwa lakini kuna baadhi ya mazao yanaweza kuwakomboa wakulima nayo ni mahindi labda na waliolima pamba. Mpunga wanaoweza kupata katika maeneo yasiyopitika maji. Pembezoni mwa mabwawa imekuwa changamoto kubwa maana maji yamekuwa mengi hata katika usawa wa kiuno, wakati mpunga una urefu wa kidole cha mtu, imekuwa changamoto.

Wakati eneo la kata ya Ketaketa kukiwa na changamoto hizo za kukatika kwa daraja, na uhalibifu unaofanywa na mvua kubwa inayonyesha kwa kuzisomba mbegu zao wakulima zilizopandwa lakini pia kupatikana mitandao ya simu imekuwa sindano nyengine ya moto inayochoma katika kidonda kibichi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...