Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Joseph Kamonga ameishukuru serikali kwa kuzidi kutoa fedha na kuhakikisha ujenzi wa barabara ya Ludewa unakamilika ili kuwasaidia wananchi wa jimbo hilo.
Kamonga ametoa shukrani hizo wakati baadhi ya wataalamu kutoka wakala wa barabara Tanzani (TANROADS) walipotembelea na kukagua ili kujua maendeleo ya ujenzi wa bara bara kwa kiwango cha zege unaoendelea wilayani humo katika kipande cha Lusitu- Mawengi.
“Kwanza niwahakikishie wananchi kwamba kile nilichowaahidi nitasimamia kwenye hii barabara nimekifanya,kwasababu asilimia 60 zimekamilika wakati wangu.Ninamshukuru sana Mh,Rais na serikali kwa kunisikiliza nilipopigia kelele bungeni maana waliponisikiliza mimi maana yake wamewasikiliza wananchi”alisema Kamonga
Kamonga ameongeza kuwa“Wakati naanza ubunge hii barabara ujenzi ulikuwa umefikia 21% pekee,wakandarasi walikuwa wanadai madeni Makubwa sana tunaishukuru serikali kwa kuwalipa na sasa wamekwishajenga KM45 kati ya KM50 za zege”
Aidha Kamonga amesema licha ya kuendelea kumaliziwa kwa ujenzi wa kipande hicho cha bara bara kilichofikia 86% huku kikitajwa kughalimu zaidi ya Bilioni 179 mpaka kukamilika kwake mwezi Agost Mwaka huu lakini anayofuraha kubwa zaidi baada ya serikali kuongeza ujenzi mwingine wa barabara ya zege KM50kwa kipande cha Itoni-Lusitu
“Ninafurahi kuwaeleza wananchi wa Ludewa kwamba kipande cha kutoka Lusitu mpaka Njombe kilomita hamsini na zenyewe zinakwenda kujengwa kwa kiwango cha zege kama ya Lusitu –Mawengi.Na tayari mkandarasi ameshapatikana”Alisema Kamaonga
Kwa upande wake mhandisi kutoka wakala ya barabara TANROADS mkoa wa Njombe Vicent Shirima amesema mradi wa Lusitu-Mawengi ni kipande kinachojumuisha mradi mkubwa wa kutoka Itoni upande wa Njombe kwenda mpaka Manda unaojumuisha KM 211 utakuwa na manufaa makubwa kwa wakazi wa Ludewa.
“Mradi huu unatarajiwa kunufaisha wananchi wananchi na wakazi wa huku kwa kusafirisha mazao ya shambani pamoja na mbao kwani kipande hiki kilikuwa ni kipande korofi sana”alisema Shirima
Kwa upande wao wananchi wa Ludewa wanaishukuru serikali kwa kuzidi kuwasaidia kutatua chanagmoto hiyo huku wakipongeza wakala ya barabara TANROADS mkoa wa Njombe kwa kuwasimamia vema wakandarasi.
Mbunge wa Ludewa Joseph Kamonga akizungumzia ujenzi wa barabara ya Ludewa na namna ambavyo inasaidia kutatua changamoto ya wananchi wa LudewaVicent Shirima Mhandisi kutoka wakala ya barabara TANROADS mkoa wa Njombe akieleza maendeleo ya ujenzi wa barabara kipande cha Lusitu-Mawengi
Muonekano wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha zege wilayani Ludewa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...