Na Muhidin Amri, Songea

JUMLA ya mashauri 66 yamesikilizwa kwa njia ya mtandao(Video Conference) kati ya hizo Mahakama kuu imesikiliza 41,Mahakama ya  Hakimu mkazi  Songea imesikiliza mashauri 24 na Mahakama ya wilaya kesi 1.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Songea Sekela Moshi amesema hayo jana wakati  akihadhimisha kilele cha wiki ya sheria nchini iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kanda ya Songea.

Jaji Moshi alisema,usikilizaji wa mashauri kwa njia ya mtandao ni moja ya mafanikio makubwa  tangu Mahakama ilipoanza kusikiliza mashauri kwa mtandao mwaka 2019.

Alisemautaratibu wa kusikiliza mashauri kwa njia hiyo ni mzuri kwa kuwa mtu halazimiki kusafiri umbali mrefu kuhudhuri katika shauri Mahakamani na umepunguza gharama  zinazo ambatana na uendeshaji wa mashauri pamoja na kuokoa muda  kwa wadaiwa na mahakama.

Aidha Alisema, mashauriambayowashitakiwawako gerezani,ut aratibu huu umelipunguzia jeshi la magereza gharama za usafirishaji na ulinzi wa washitakiwa ikilinganishwa na utaratibu wa awali uliokuwa unalazimu kuwapeleka washitakiwa hao mahakamani.

Aidha, amempongeza Mh.Rais Samia Hassan kwa jitihada za dhati na mbinu za kisasa alizozianzisha kukabiliana na janga la Uviko 19 , hivyo amewataka watumishi wote wa mahakama kanda ya songea na wananchi kwenda kupata chanjo kwani ni muhimu katika mapambano ya uviko.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya songea Pololet Mgema alisema Mfumo wa usikilizaji kesi kwa njia ya Mtandao umesaidia kupunguza kesi na kukomesha vitendo vya uombaji Rushwa kwa watendaji wa mahakama kwani hawakutani.

NayeMwenyekiti wa chama cha Wanasheria wa Tanganyika chapter ya Ruvuma Edson Mbogoro alisema,utawala wa sheria huwasaidia watu kushiriki katika mapambano ya kukabili vitendo dhalili vya rushwa ,matumizi mabaya ya madaraka  na ukandamizaji wa raia wasio na hatia.

Aliongeza kuwa utawala wa sheria unajenga na kusimamia taasisi imara za kuendesha  nchi kwa misingi ya haki ,kudumisha tamaduni wa kuheshimu sheria.

Mkazi wa Songea Onesmo Mlowe, amewataka watendaji wa mahakama kuendelea kutoa haki kwa wananchi na kuacha kudai rushwa kwa  wananchi wengi wa vijijini hawajui sheria.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea Mheshimiwa Sekela Moshi akizungumza na watumishi na wageni waalikwa katika maadhimisho ya siku ya sheria iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda yA songea.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda y Songea Mheshimiwa  Sekela Moshi akikagua gwaride la Heshima kuadhimisha siku ya sheria nchini iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Songea.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...