Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe 04 Februari 2022 akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole uliopo Addis Ababa, Ethiopia na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Balozi Birtukan Ayano. Makamu wa Rais yupo nchini Ethiopia kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaotarajiwa kufanyika tarehe 5 na 6 Februari 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...