**************************
Na. John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Mohamed Mchengerwa amemtembelea aliyekuwa Mbunge wa Mikumi na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Bw. Joseph Haule (Prof. Jay) anayetibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mhe. Mchengerwa amefika leo Februari 12, 2022 kumjulia hali msanii huyo na kuwasilisha salamu za Serikali kama msimamizi Mkuu wa Sekta ya Sanaa hapa nchini.

“Nimefika kumjulia hali mmoja wa wadau na miongoni mwa wasani ambao tunatambua na kuthamini mchango wa kazi zake za sanaa ambazo zimehamasisha vijana wengi kujiajiri kupitia Sanaa ya muziki hapa nchini”. Ameeleza Mhe. Mchengerwa

Tayari Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema itagharamia matibabu yake hadi hapo ataporuhusiwa kutoka hospitalini hapo.

Kwa upande wake mke wa Prof. Jay, Bi. Grace Mgonjo amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa upendo wa kuja kumwona msanii huyo .

Pia ameushukuru Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuwapokea na kuwahudumia vizuri.

Katika hatua nyingine Waziri Mchengerwa amewapongeza madaktari na wauguzi wa Hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanayofanya ya utoaji wa matibabu ya kibingwa kwa Watanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...