Na Janeth Raphael - Dodoma

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema wabunge 19 wa Viti Maalum wa Chadema waliopo bungeni wapo humo kihalali.

Hata hivyo amesema anasubiri michakato halali ndani ya chama chao na ngazi zingine ikithibitika hakuna shida atatekeleza takwa la kikatiba.

Novemba 2020 waliapishwa wabunge 19 wa Chadema ambao walizusha malumbano ya namna waliteuliwa na majina yao kupelekwa Bungeni kwani chama chao hakikutoa ridhaa.

Spika Dk Tulia ametoa kauli hiyo leo Jumatatu februari 14, 2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na Wahariri na waandishi wa habari wanaoripoti Bunge.

Akijibu swali kuhusu uhalali wa wabunge wao, Spika amesema hadi sasa wabunge hao wapo kwa mujibu wa sheria kwani kila mbunge ni lazima atokane na chama na hao nao wametokana na chama.

Amesema Bunge halioni shida kuwaondoa wabunge na lilishawahi kufanya hivyo katika mabunge yaliyotangulia.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...