•Apata fursa ya kujitambulisha kwa watoa hudum
•Atoa tuzo na zawadi kwa wafanyakazi bora wa robo ya mwisho ya mwaka 2021

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose (kulia) akipata maelezo ya namna wateja wanavyohudumiwa kutoka kwa Meneja Uendeshaji wa kituo cha huduma kwa wateja Vodacom, Jombo Mkono wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea kituo hicho kilichopo mlimani city jijini Dar es Salaam ili kujitambulisha na pia kuona mambo mbalimbali.


Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,  Rosalynn Mworia (kulia) na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja, Harriet  Lwakatare  (kushoto) wakati mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo alipotembelea kituo cha huduma kwa wateja kilichopo Mlimani city jijini Dar es Salaam na kutoa tuzo na zawadi kwa wafanyakazi bora wa robo ya mwisho ya mwaka 2021 na kuwaasa kuzingatia maadili na kutoa huduma bora zaidi.


Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose akimkabidhi cheti Erick Mkunda kwa kutambua mchango wake katika kuhudumia wateja wa kampuni ya Vodacom

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose akizungumza na wafanyakazi wa kituo cha huduma kwa wateja Vodacom kilichopo Mlimani city jijini Dar es Salaam na kutoa tuzo na zawadi kwa wafanyakazi bora wa robo ya mwisho ya mwaka 2021 na kuwaasa kuzingatia maadili na kutoa huduma bora zaidi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...