Akizungumza na Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) wakati wa kutoa mafunzo hayo Afisa wa NBAA kutoka Idara ya Elimu na Mafunzo, Ibrahim Magambo amesisitiza kuwa si kila aliyesomea uhasibu anaweza kufanya kazi za kihasibu bali inabidi kufanya mitihani ya Bodi hiyo ili kupewa cheti cha kitaaluma ili uweze kutambulika kama Mhasibu na kuweza kufanya kazi nje na ndani ya nchi, wanafunzi wa Kozi nyingine ambazo hazihusiani na masomo ya Uhasibu nao wana nafasi ya kufanya mitihani ya Bodi na wataanzia masomo ya ngazi ya kwanza (foundation level) tofauti na wale waliosomea masomo ya Uhasibu na pia waliomaliza kidato cha nne na sita na wanacheti wanaweza kufanya mitihani ya Bodi
Afisa wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) kutoka Idara ya Elimu na Mafunzo, Ibrahim Magambo akitoa elimu kwa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) jijini Dar es Salaam ikiwa ni lengo la kutoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo kwa Taasisi, Vyuo pamoja na Shule za Sekondari.
Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA Magreth Kageya akitoa ufafanuzi kuhusu kazi zinazofanywa na bodi hiyo wakati wa mafunzo kwa Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) wakifuatilia mada kutoka ka maofisa wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) waliofika chuoni hapo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo pamoja na namna ya kuweza kupata CPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...