Na Amiri Kilagalila,Njombe
Timu
ya Chama la wana ya mjini Makambako mkoani Njombe imetwaa kombe la B2K
cup katika michuano hiyo iliyodhaminiwa na kampuni ya shikamoo
Parachichi na kukabidhiwa zawadi ya Ng'ombe baada ya kuifunga timu ya
jeshi la polisi Makambako kwa mikwaju ya penati 4 kwa 3.
Akizungumza
wakati akikabidhi zawadi mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Njombe
Bi Kissa Kasongwa amemshukuru mkurugenzi wa shikamoo parachichi Erasto
Ngole kwa kudhamini ligi hiyo na kuhakikisha vijana wanakusanyika pamoja
na kudumisha amani na upendo kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Mkuu
wa wilaya hiyo amekabidhi Ng'ombe kwa mshindi wa kwanza wa ligi hiyo
ambayo ni timu ya chama la wana,huku mshindi wa pili timu na polisi
Makambako ikikabidhiwa mbuzi wa wiwili na Mshindi wa tatu Goldeni
ballers imekabidhiwa mpira huku marefa,mfungaji bora,mchezaji mwenye
nidhamu wote kwa pamoja wamekabidhi zawadi pia.
Balozi
wa kampuni ya shimoo Parachichi ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za kizazi
kipya Batwery kinyunyu (B2K) amemshukuru mkuregenzi huyo Ngole kwa
kudhamini ligi hiyo na kueleza kuwa lengo kubwa la ligi hiyo ilikua ni
kuhamasisha vijana kujiajiri katika kilimo cha parachichi ambacho
kimekua na tija kubwa mkoani njombe .
Licha
ya kudhamini ligi hiyo mkurugenzi wa kampuni ya shikamoo Parachichi
Elasto Ngole ambaye ni katibu wa siasa na uenezi (CCM) mkoa wa Njombe
ameahidi kutoa zaidi ya milioni tatu ili kuhakikisha msanii huyo B2K
ananunua camera ambazo zitamuwezesha kufungua studio ya kurekodia video
ili aweze kuwasaidi vijana wote ambao wanajihusisha na tasnia hiyo ya
uimbaji wa nyimbo za kizazi kipya na zile za injili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...