Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetoa taarifa kwa umma kuhusu wanachama wa wapya 2,194 watakaopatiwa vyeti vya usajii na Bodi hiyo.
Akitoa taarifa hiyo Meneja Masoko na Uhusiano wa PSPTB, Shamim A. Mdee amesema vyeti vya usajili wa taaluma kwa wanachama 1,163 wa tarehe 24 Julai mwaka 2020 vitanza kutolewa kuanzia kesho Februari 04 mwaka 2022 katika ofisi za Bodi hiyo zilizopo Keko Mwanga mkoani Dar es Salaam.
Pia amesema jumla ya wanachama 1,031 waliopata namba ya usajili tarehe 19 Januari mwaka 2022 wanajulishwa kuwa vyeti vyao vitakuwa tayari kuanzia tarehe 20 Februari mwaka 2022 na pia wanachama waliopo nje ya Dar es Salaam wanaombwa kuwasiliana na Bodi hiyo kwa namba +255738442971 kwa ajili ya kupatiwa muongozo wa jinsi ya kupata vyeti vyao..
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) inawakumbusha wanachama wake wote waliolimbikiza asa za mwaka kukamilisha malipo yao pindi wapatapo taarifa hii na pia Bodi hiyo inawasisitiza wanachama wapya kuwa vyeti vitatolewa kwa wanachama waliokamilisha malipo ya ada kwa mwaka wa fedha husika tu. Alisema Mdee
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...