Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi wa Kituo cha kuwezesha Wajasiriamali cha Station F Start Up Bi. Roxanne Varza pamoja na Meneja Mawasiliano wa Kituo hicho Bw. Grégoire Martinez kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa Kituoni hapo ikiwemo kutoa fursa kwa wajasiriamali wadogo kupata elimu ya ubunifu wa kibiashara, fursa za mitaji yenye masharti rafiki pamoja na masoko wakati alipotembelea Kituo hicho leo tarehe 12 Februari, 2022, Paris nchini Ufaransa)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi wa Kituo cha Station F Start Up facility Bi. Roxanne Varza kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa Kituoni hapo mara baada ya kukitembelea leo tarehe 12 Februari, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na baadhi ya Wabunifu na wafanyabiashara katika Kituo hicho cha Station F Start Up facility mara baada ya kukitembelea Kituo hicho Paris nchini Ufaransa leo tarehe 12 Februari, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na kituo cha Station F Start Up facility mara baada ya kukitembelea Kituo hicho Paris nchini Ufaransa leo tarehe 12 Februari, 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...