- Avikabidhi kwa kila Halmashauri kwaajili ya kutumika hospitalini.

- Asema msaada huo Ni Matokeo ya jitiada za Rais Samia Suluhu Hassan kudumisha mahusiano ya Kidiplomasia.

- Kontena nyingine 6 za Vifaa kutua nchini wakati wowote.

Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amepokea msaada wa Vifaa vya afya ikiwemo Vitanda na Meza vyenye thamani ya Shilingi Milioni 205 kutoka Jiji la Hamburg ya Ujerumani kupitia Taasisi ya The Free Hanseatic city Dada wa Jiji la Dar es salaam.

RC Makalla amesema kupatikana kwa Vifaa hivyo Ni Matokeo ya jitiada anazofanya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha mahusiano ya Kidiplomasia baina ya mataifa mbalimbali.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa hivyo iliyofanyika hospital ya Wilaya ya Kigamboni, RC Makalla amesema msaada uliotolewa awali Ni Kontena 3 zenye Vitanda 108 na Meza 72 na awamu ya pili zitakuja Kontena 6 zenye vitanda 324, vitanda 151 vya wagonjwa mahututi na Meza 51.

Aidha RC Makalla Baada ya kupokea Vifaa hivyo amevikabidhi kwa Halmashauri za Dar es salaam ambapo Wilaya ya Kigamboni imepokea Vitanda 24 na kabati 16, Kinondoni vitanda 21 na kabati 14, Temeke vitanda 21 na kabati 14, Ilala vitanda 21 na kabati 14 na ubungo vitanda 21 na kabati 14.

Hata hivyo RC Makalla amesema msaada wa vitanda hivyo umekuja wakati muafaka na vitasaidia kupunguza Kero ya uhaba wa vitanda hospitalini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh , Amos Gabriel Makalla akikata utepe kuashiria kupokea rasmi vitanda kutoka Ujerumani

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akiwa na Viongozi mbalimbali wa mkoa pamoja na wakuu wa Wilaya wakikagua shehena ya Vitanda vilivyoifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya KigamboniMtaalamu wa Vifaa tiba akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Amos Makalla namna vitanda hivyo vinavyofanya kazi na vinavyoweza kumsaidia mgonjwa kwa urasi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. YouTube | Live Video and TV production - Vimeo
    YouTube is a free service youtube to mp3 free of Vimeo that offers instant access to all the most popular channels in the industry including the big names in the music industry.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...