Na. Angela Msimbira MBEYA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amesema serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Tembela ili kutatua changamoto ya miundombinu ya barabara na madaraja katika eneo hilo.
Akikagua miundombinu ya barabara katika kata ya ya Tembela , Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya leo tarehe 15 Februari,2022 amesema ujenzi wa Daraja la Tembela litasaidia kuunganisha wananchi wa Kata ya Mwasanga, Mwakibete, Tembela na Mbeya vijijini ambao walikuwa wakipata adha ya Mawasiliano ya barabara tangu daraja hilo lilipobomoka mwaka 2019 na kusababisha vifo vya watu watano katika eneo hilo.
Waziri Bashungwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani kwa kutoa fedha hizo na kusikiliza kilio cha wananchi wa kata hizo ili kutoa nafuu ya mawasiliano ya barabara katika eneo la Mbeya Mjini na Vijijini.
Amemuagiza Meneja wa TARURA Mkoa wa Mbeya Mhandisi Charles Mwita kuhakikisha Mkandarasi anaanza ujenzi wa Daraja hilo ifikiapo Tarehe 1 Machi, 2022 na kuhakikisha anatuma picha mnato na video zinazoonyesha ujenzi huo umeanza kufanyika.
Waziri Bashungwa amemuagiza Meneja huyo kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ujenzi huo ili dhamani ya fedha zilizotolewa na serikali zinatumika na kupata dhamani ya fedha iliyotolewa ziendane sambamba na ubora wa ujenzi wa miundombinu ya daraja hilo.
Amesema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha inatatua changamoto za miundombinu ya barabara kwa wakati na kurejesha mawasiliano katika kata husika ili kuinua uchumi wa kata hizo.
Aidha amewashukuru wananchi kwa kuendelea kuunga mkono serikali kwa kujitolea kuweka madaraja mbadala lengo likiwa ni kuhakikisha madaraja hayo yanapitika na wananchi wanaendelea kupata huduma.
Naye Diwani kata ya Tembela Fred Kibeso Mwasoke amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo ambalo linaunganisha maeneo ya Mwasanga, Mwakibete, Matembele na vijiji vinavyozunguka, kwa kuwa wanaamini kuwa uchumi utafunguka.
Home
HABARI
Serikali yatoa shilingi Bilioni 1.4 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Tembela, Jijini Mbeya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...