Na Mwandishi wetu, Babati

MIRADI ya maendeleo 82 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.6 imefuatiliwa na dawati la uzuiaji rushwa kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara.

Kamanda wa TAKUKURU wa Mkoa wa Manyara, Holle Joseph Makungu, ameyasema hayo mjini Babati wakati akizungumza kupitia taarifa yake ya miezi mitatu iliyopita.

Makungu amesema kwa mujibu wa ufuatiliaji huo, mingi ya miradi hiyo imekuwa ikitumia njia ya manunuzi kupitia ‘force account’ na mingi iliyotembelewa inaakisi thamani ya fedha.

Hata hivyo, amesema katika ufuatiliaji huo walibaini kuwepo kwa baadhi ya wakandarasi wanaoomba ujenzi wa miradi hiyo kuwa na mafundi wa mitaani wanaoomba kazi kwa bei inayowawezesha kuwashinda washindani ila baadaye huanza madai ili wapate mapato ya ziada.

“Ni rai yetu kwa wakurugenzi wa halmashauri kuwa macho na watu wa aina hiyo ikizingatia kuwa utekelezaji wa miradi ya serikali kwa utaratibu wa kutegemea mafundi wa mtaani unaendelea kufanyika,” amesema Makungu.

Amesema wananchi wanapaswa kutoa taarifa kwao TAKUKURU endapo watabaini kuna matendo machafu yanafanyika kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo katika vijiji, mitaa au kata zao. 

“Rai yetu kwa wana Manyara ni kuwaomba kuendelea kutoa taarifa za rushwa na wanaojihusisha na vitendo hivyo, kupitia namba yetu ya dharura 113 au kwa kufika katika ofisi zetu zilizopo karibu nao, kama sehemu ya kuunga mkono kauli mbiu ya kupambana na rushwa ni jukumu langu,” amesema Makungu.

Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza na waandishi wa habari Mjini Babati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...