Na. John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali ya  Tanzania inakwenda kufufua mpango wa miaka mitatu wa maendeleo ya Sekta za utamaduni, sanaa na michezo  ulioingiwa na  Serikali ya China.

Akizungumza Februari 4, 2022 jijini Dar es Salaam na Balozi wa China nchini  Mhe. Chen Mingjian katika kikao maalum kwenye sherehe za uzinduzi wa michezo ya msimu wa baridi ya Olympic 2022 amesema tayari wizara yake imeandaa andiko kwa ajili ya mpango huo litakalowasilishwa hivi karibuni.

Katika kikao hicho Mhe. Waziri aliambatana na Katibu Mkuu wake, Dkt. Hassan Abbasi

"Tunatarajia kuwasilisha mpango wetu ambao tutaingia makubaliano ili utekelezaji wake uanze mara moja" amefafanua Mhe. Mchengerwa

Kwa upande wake Balozi Chen amesema   ni wakati mwafaka wa kufufua na kuendeleza sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuinua uchumi wa nchi zote baada ya kushuka kutokana na ugonjwa wa Uviko 19.

Amesema Serikali yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu kupitia mafunzo mbalimbali.

"Awali watu wetu walikuwa wanapata fursa ya kuja Tanzania  na watanzania kwenda China lakini kutokana uviko tulishindwa sasa ugonjwa umepita. Tunajipanga  tuinue  sekta zetu kwa pamoja" ameongeza  Mhe. Balozi Chen

Amempongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa msimamo wake wa kuendelea kuenzi na kuendeleza uhusiano mzuri uliojengwa na viongozi waasisi wa mataifa haya mawili kwa muda mrefu.




 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...