Huku zikiwa zimebaki takriban wiki tatu tu kabla ya kufanyikka kwa mbio za 20 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2022, waandaaji wa mbio hizo wamewakumbusha washiriki kuwa usajili unafungwa Jumatatu Februari 7, 2022.

Taarifa iliyotolewa jana Jijini Dar es Salaam, ilisema usajili utafungwa rasmi Februari 7, 2022 saa sita ya usiku na kuwataka ambao hawajajisajili kutumia muda uliobaki kujisajili kwa njia ya mtandao ili kuepukana na usumbufu.

“Usajili ni kwa njia ya mtandao kwa kupitia tovuti yetu ya www.kilimanjaromarathon.com au Tigo Pesa kwa kupiga *149*20#. Mtandao hautafanya kazi baada ya Februari 7, 2022 kwa hivyo ni bora watu watumie muda uliobaki kufanya usajili,” walisema waandaaji hao.

Hata hivyo walisema usajili wa mbio za Grand Malt za Km 5 maarufu kama Fun Run utaendelea hata baada ya tarehe hiyo iliyotajwa na pia katika vituo vya kuchukulia namba za kukimbilia.
“Tunapenda pia kuwakumbusha washiriki kuwa endapo nafasi zitajaa kabla ya Februari 7, 2022 basi tutalazimika kufunga usajili mara moja, ilisema taarifa hiyo ya waandaaji.
Walisema watatangaza tarehe na vituo ambapo washiriki watachukua namba za kukimbilia kwa mikoa ya Dar es Salaam,Arusha na Kilimanjaro. The organizers said that soon they will announce race number collection points and dates in Dar es Salaam, Arusha and Moshi.

Wadhamini wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2022 ni Kilimanjaro Premium Lager (Mdhamini Mkuu) Tigo (21km) na Grand Malt (5km).
Wadhamini wa meza za maji ni pamoja na Absa Tanzania, Unilever Tanzania, TPC Sugar, Simba Cement na Kilimanjaro Water. Wasambazaji rasmi ni GardaWorld Security, Keys Hotel, Kibo Palace Hotel, CMC Automobiles na Surveyed Plots Company Ltd (SPC) na Bodi ya Utalii (TTB).

Katika hatua nyingine, Kwa mujibu wa waandaaji wa Kilimanjaro Marathon, kwa mara ya kwanza kutakuweko na maonesho yanayojulikana kama Kili Expo (The People's Expo) ambapo wadhamini na wadau wengine wa mbio hizo watapata fursa ya siku tatu za kuonyesha bidhaa na huduma wanazotoa, maonyesho ambayo yanatarajiwa kufanyika kati ya Februari 24-26, 2022, katika viwanja vya MoCU.

"Maonyesho haya pia linakusudiwa kuwapa umma uzoefu wa muda mrefu wa mbio za Kili Marathon; pia kwa mwaka huu wanaotarajia kushiriki mbio hizo watapata fursa ya kuchukua namba zao za ushiriki eneo la chuo kikuu cha Ushirika badala ya eneo la hotel kama ilivyokuwa miaka ya nyuma”, ilisema taarifa hiyo ya wandaaji.

Mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, zinatarajiwa kufanyika Jumapili ya Februari 27, 2022, katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), ambapo zimeandaliwa na taasisi ya Kilimanjaro Company Limited na kuratibiwa na wadau wa hapa nchini kampuni ya Executive Solutions Limited.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...