*********************

WAKATI kampeni ya NMB MastaBata – Kivyako Vyako ikizidi kunufaisha wateja kwa washindi 25 wa mwezi wa kwanza wa kampeni hiyo kuzawadiwa Sh. Mil. 25, msisitizo umetolewa kwa Watanzania kuwa matumizi ya pesa taslimu ni gharama ‘cash is expensive,’ na kwamba MastaBata ikawe chachu ya kudumisha utamaduni wa matumizi kwa njia ya kadi.

MastaBata ni kampeni inayoendeshwa na Benki ya NMB, ikihamasisha Watanzania kuendana na kasi ya dunia ya dijitali, ya matumizi ya yasiyohusisha pesa taslimu, huku benki hiyo ikitenga zaidi ya Sh. Mil. 200 kama motisha kwa wateja wanaotumia zaidi kadi zao za MasterCard, Masterpass QR, Vituo vya Mauzo (PoS).

Kufikia sasa, kampeni hiyo iliyoanza mwishoni mwa Desemba mwaka jana, imeshatoa zawadi za pesa taslimu kiasi cha Sh. Mil. 65 kwa wateja 425, ambazo ni kati ya zaidi ya Sh. Mil. 200, zitakazotolewa kwa wateja 1,080 katika kipindi cha wiki 10 za kampeni hiyo, inayofanyika kwa msimu wa tatu. Fainali ya NMB MastaBata itafanyika Machi mwaka huu.

Akizungumza kabla ya droo hiyo, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, alisema ulimwengu umebadilika na kusisitiza kuwa matumizi ya pesa taslimu yana gharama kubwa, zikiwamo za upotevu, wizi na uporaji na kwamba Watanzania wanapaswa kuendana na kasibya mabadiliko hayo kwa kujikita katika matumizi kwa njia ya kadi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo Cha Wateja Binafsi wa NMB, Aikansia Muro, alisema benki yake imetenga zaidi ya Sh. Mil. 200, zitakazotolewa kwa wateja wao katika kipindi chote cha kampeni hiyo, ambako kila wiki wateja 100 hujinyakulia jumla ya Sh. Mil. 10 (sawa na Sh. 100,00 kila mmoja), huku washindi 25 wa kila mwezi wakijitwalia Sh. Milioni 25 (sawa na Sh. Mil. 1 kila mmoja).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...